Huenda ikawa ni ajabu kwa watu kusikia kucha zinaweza kutumika kama kitega uchumi na kuendesha maisha ya binadamu.Lakini jambo hili limeweza kuthibitishwa na raia mmoja wa Kenya aitwaye John Waweru ambaye amekuwa akifuga kucha zake kwa miaka kumi na mbili sasa.Akizungumza na gazeti la
Nairobi news kijana huyo amesema hadi hivi sasa kucha zake zina urefu wa futi moja na inchi tatu na kuwa aliamua kuacha kazi aliyoipata ili kufuga kucha hizo ambazo anaonekana kuzipenda.Aliongeza zaidi kuwa uamuzi wake huo hivi sasa umemfanya kunufaika kufuatia watalii kujitokeza na kuanza kumlipa kwa kuzitazama na wengine kupiga naye picha.Pia alieleza zaidi kuwa kufuatia hali hiyo aliamua kuzipaka rangi za bendera ya nchi yake ya Kenya hali ambayo imeonesha kjwavuta zaidi watalii na kuwa humuwezesha muingiza kiasi cha zaidi ya shilingi elfu tisini za kitanzania pindi biashara ikiwa nzuri.




Axact

Post A Comment: