Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Mmiliki wa shindano la
Bongo Star Search nchini Tanzania Rita Paulsen maarufu kama madam Rita ameamua
kuwafungukia baadhi ya watu ambao wwanaitumia mitandao ya kija mii vibaya.
Kupitia ukurasa wake wa
face book mama huyo ameandika maelezo yanayoashiria kupinga watu hao ambao mara
nyingi huchafua majina ya watu kwa kuandika vitu visivyo faa.
“Hivi
sasa mitandao ya kijamii inawezesha watu kusema kile wanachokifikira na kutaka
sauti na hoja zao kusikilizwa. Lakini wengine wamekuwa wakitumia mitandao ya
kijamii kutusi na kuchafua majina ya watu. Huo kwakweli sio uungwana kwani
hamna faida yoyote itakayopatikana pindi unapomchafulia mtu mwingine jina lake.
Ni mtazamo tu!. Nawatakia Alhamisi njema wadau” Aliandika Madam Rita
Ni mtazamo tu!. Nawatakia Alhamisi njema wadau” Aliandika Madam Rita
Imekuwa
ni kwaida kwa baadhi ya watu kuchafua watu au kupost picha mbaya katika
mitandao ya kijamii kiasi cha kusumbua watu wengine.