2014-04-27
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Kijana mmoja mwenye(26) anayetanbulika kwa jina la David Campaya amekamatwa na polisi nchini Hispania kwa kitendo cha kibaguzi alichokionesha kwa mchezaji wa Barcelona Daniel Alves kwa kumtupia ndizi. Taarifa kutokaa katika club ya Viller real anayoiunga mkono zinasema  club hiyo imemfungia kutazama mechi zilizosalia na kuwa imemfungia maisha.Kitendo hicho cha kutupa ndizi kimechukuliwa kwa mtazamo hasi na watu wengi dunian ambapo wameonesha kumuunga mkono Alves kwa kitendo cha kuila ndizi ile ambapo watu wengi wamekuwa wakipost picha katika mitandao ya kijamii zinazowaonesha wanakula ndizi.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Huenda hali hii ikawa fundisho kwa baadhi ya viongozi hapa nchini ambao wamekuwa wakitajwa kuwa miongoni mwa watumiaji wa vilevi na pia kuonekana katika club za usiku.Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC Meya wa mji wa Toronto Rob Ford ambaye amekuwa akijikuta katika mazingira magumu kufuatia utumiaji wake wa vilevi na mihadharati ameripotiwa kujitambua na kupanga kuchukua likizo ili kufanyia kazi tatizo hilo.Taarifa kutoka kwa mwanasheria wa meya huyo Bw.Denis Moris zinasema tayari meya huyo amekwisha tambua tatizo linalomdhalilisha na kuwa atachukua likizo ili kulifanyia kazi.Uamuzi huu wa meya huyo unakuja katika wakati ambao magazeti mawili ya Canada yakidai yamepata kanda mpya ya inayomuonesha meya huyo akiwa amelewa na akitoa maneno mabaya kww wanawake na wanasiasa wenzake. Habari zaidi zinasema meya huyo bado anampango wa kutetea nafasi yake katika uchaguzi October mwaka huu.






Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Baadhi ya wapenzi wa muziki na burudani kwa ujumla jijini Mwanza wameonesha kukubali alichokifanya msanii toka nchini Uganda Dr.Jose Chameleon.Wakizungumza na bingo 20 mashabiki hao wamelisema Chameleon alifanya kitu kikubwa kiasi cha kuwaridhisha mashabiki wake.Waliongeza kuwa alichokifanya kinaonesha kuwa alijiandaa na kuwashauri wasanii wa hapa nchini kuongeza juhudi zaidi wawapo jukwaani.


Chemeleon akiwapagawishaa mashabiki







Chameleon akiwa na kiongozi wa bendi inayotumbuinza Villa park

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amesema atatumia nguvu kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wanaopanga bidhaa zao katika maeneo yasiyoruhusiwa.

 Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika mapema jijini Mwanza mapema wiki hii Ndikilo alisema walikwisha fanya mazungumzo na wafanya biashara hao ili waondoke lakini zoezi hilo halijafanikiwa.
 Kufuatia hali hiyo alieleza hakuna namna zaidi ya kuwaondoa kwa nguvu akitumia jeshi la polisi. Kwa upande wake kaimu kamanda wa polisi mkoani Mwanza Christopher Fuime alisema kabla ya kuanza kuwaondoa watatoa matangazo ya kuwataka waondoke na kisha kuwatoa kwa nguvu wala watakao kaidi.








Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Wafanya usafi wa barabara na madampo jijini mwanza wapo katika hatari ya kuathirika kiafya kutokana na baadhi yao kufanya shughuli hiyo bila ya kuwa na vifaa vinavyotakiwa.
Akizungumza na Afya radio bi Amina Almas mmoja wa wafanya usafi jijini humo alisema wengi wao wanakabiliwa na upungufu wa vifaa kama gloves,viatu vya usalama na vifaa vya kuzuia vumbi ambapo alieleza kuwa baadhi yao wanavyo na wengine bado hawajapatiwa.
Alieleza kuwa hulazimika kuzoa taka kwa mikono na vifaa visivyo rasmi kama ubao ambapo hukutana na changamoto ya kukutana na vinyesi na hata wanyama waliogongwa na vyombo vya usafiri.
Kwa upande wake Afisa afya wa jiji la Mwanza Bw. Danford Kamenya alisema wao kama wasimamizi wa masuala ya afya wanafanya jitihada za kuwabana mawakala wa usafi ambao ndio waajii wa wafanya usafi hao ili kufuata taratibu zinazotakiwa
Vilevile Bw. Kamenya aliwaomba wafanya usafi huo walio na vifaa kuvitumia na sio kuviacha nyumbani


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Huenda ikawa ni ajabu kwa watu kusikia kucha zinaweza kutumika kama kitega uchumi na kuendesha maisha ya binadamu.Lakini jambo hili limeweza kuthibitishwa na raia mmoja wa Kenya aitwaye John Waweru ambaye amekuwa akifuga kucha zake kwa miaka kumi na mbili sasa.Akizungumza na gazeti la