Mwimbaji wa ‘Tumetoka Mbali’, Linah Sanga ambaye aliahidi kuanzisha kipindi cha runinga mwezi wa nane mwaka jana, ameelezea sababu zilizompelekea yeye kushindwa kuitimiza ahadi hiyo kwa muda.
Akizungumza na muandishi wa tovuti ya Times Fm alisema alishindwa kutekeleza ahadi hiyo kwa wakati kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza kwa upande wa uongozi wake, ulioshauri kubadilika kwa ratiba hiyo, “Mimi na timu yangu (Crew) tulitegemea kukirusha hewani mwaka Jana ila uongozi uliona ni vizuri tuanze rasmi kukirusha mwaka huu.”
Amesema kipindi hicho cha Television alichokipa jina la 3D, kina lengo la kuwahamasisha wazazi wote nchini kutowalemaza watoto wao kwenye vipaji tu na kusahau masomo kwa kuwa anaamini elimu ndio msingi wa maisha bora.
Endapo kipindi hicho kitaanza, Linah ataingia kwenye orodha wasanii wa Tanzania wenye vipindi vyao binafsi kwenye vituo vya runinga wanaoshiriki moja kwa moja na kuonekana, kama Lady Jay Dee, Wema Sepetu na wengine.
Post A Comment: