Watu wengi wamekuwa wakiendelea kukumbwa na tatizo la kuoza kwa meno na kujikuta wakiishia kuwa na mapengo bila ya kujua chanzo cha kuharibika kwa meno hayo.
Kwa mujibu wa kaimu mgamga wa meno mkoa wa Mwanza Dr. Ismail Sarumbo wakati akifanya mahojiano na Muandishi Charles Urio katika kipindi cha Linda Afya yako cha Afya radio Mwanza alibainisha kuwa tatizo hili husababishwa na bacteria wa aina tofauti tofauti ambao kwa pamoja wanaitwa normal Flora wanaoishi katika mdomo wa binadamu.
Bakteria hao huharibu jino kwa kemikali ambayo wameitengeneza baada ya kukutana na mabaki ya vyakula katika meno.
Watu wengi hukumbwa na hali hii kutokana na kutokuwa na tabia ya kupiga mswaki mara baada ya chakula hali ambayo inaacha mabaki ya chakula katika meno hali ambayo inatufanya tuyaathiri meno yetu wenyewe.
Ili kuepuka ugonjwa huu hatuna budi kuchukua hatua ya kupiga mswaki mara kwa mara pindi tunapo maliza kula na kuyaaacha meno yetu yakiwa salama.
Kwa undani zaidi Download na umsikilize kaimu mganga wa meno Dr. Ismail Sarumbo

Axact

Post A Comment: