2014-03-16
no image
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Mshiriki wa Big Brother Africa ‘The Chase’, Huddah Monroe wa Kenya ameendelea kumchana Mustapha ambaye awali walitangaza kuwa na uhusiano na mwisho Huddah kubadilika na kudai yote yale yalikuwa yamepangwa tu ili kumpa ‘kick’ Mustapha.
Huddah ambaye hivi karibuni alidai kuwa Mustapha sio tabaka lake ‘not my class’, usiku wa jana aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akidai tabaka la wanaume anao-date nao wako busy wanataka kuingia kwenye orodha ya jarida la Forbes ambalo ni jarida maarufu zaidi duniani kwa kupanga viwango vya watu wenye mafanikio, na kuonesha kumshangaa Mustapha kwa kudai yeye yuko busy anatafuta umaarufu kwenye mitandao ya kijamii.
“The class of men I date are busy out there looking to be on Forbes list not busy looking for social media fame!!!!! Hehe! Never seen a man so bitter over a woman he only saw half naked a photo shoot….Chill, at least u got to take to floss with!” aliandika Huddah ambaye aliifuta post yake muda mfupi baadae.
Mustapha nae allimjibu kwa kejeli kuwa akapige picha na Bill Gates.
“I have moved on, I suggest she does the same,Next time, she should be wise n not leave photographic evidence! Ati anadate jamaa class ya forbes? haahahahahaha akapige picha na Bill Gates!" Amesema Mustapha.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Mamlaka ya udhibiti wa safari za nchi kavu na majini (sumatra) imevitaka vyombo vyote vya usafiri hasa vya  majini kuzingatia kanuni za ubabebaji wa mizigo wakati wa safari.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya abiria watumiao usafiri wa meli kulalamikia vitendo vya meli za kwenda bukoba kujaza mizigo kupita kiasi hali inayotishia usalama wa safari zao.
Akizungumza na afya radio  afisa mfawidhi wa sumatra kanda ya ziwa japhert ole loisumaye alisema ubebaji wa mizigo unatazamwa kwa kupimwa na vifaa maalum  na wala si kwa kukadilia
Akizungumzia tatizo la kuchelewa kuondoka bandarini meli ya mv victoria loisumaye amesema wakati mwingine ni hali ya hewa ndio inachangia
Mamlaka ya udhibiti wa nchi kavu na majini inawaomba wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo endapo wataona vyombo vya usafiri vinavunja kanuni na sheria za usafirishaji.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Jaji wa Los Angeles ametoa uamuzi wa kuendelea kwa kesi ya Kanye West na Kim K dhidi ya mmoja kati ya waanzilishi wa YouTube, Chad Hurley aliyevujisha video ya tukio la wawili hao kuvishana pete.
Mara ya kwanza Jaji wa mahakama ya California alisitisha kwa muda kuendelea kwa kesi hiyo baada ya Chad Hurley kudai kesi hiyo dhidi yake ifutwe kwa kuwa katiba inamlinda kwa madai kuweka kipande cha video hiyo ilikuwa sehemu ya ‘haki/uhuru wa kujieleza’.
Hurley alifunguliwa mashtaka siku moja baada ya kuweka kwenye mtandao wake wa MixBit kipande cha video ya tukio hilo lililofanyika October mwaka jana, kinyume na makubaliano au masharti yaliyowekwa na Kanye West na Kim Kardashian kuwa picha wala video hazirusiwi kuchukuliwa wakati wa tukio.
Katika mashtaka hayo, Kanye West na Kim Kardashian wamedai kuwa Hurley alivunja makubaliano ya usiri yaliyowekwa na kwamba inawezekana amevunja haki ya waandaaji wa show ya ‘Keeping Up With The Kardshians’ ambao walikuwa wanakibali cha kushuti tukio hilo na kulionesha kwenye kituo cha runinga cha E!
Kim Kardashian na Kanye West wanataka walipwe fidia ambayo bado hawajataja kiwango. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 17, Mwaka huu.