Mshiriki wa Big Brother Africa ‘The Chase’, Huddah Monroe wa Kenya ameendelea kumchana Mustapha ambaye awali walitangaza kuwa na uhusiano na mwisho Huddah kubadilika na kudai yote yale yalikuwa yamepangwa tu ili kumpa ‘kick’ Mustapha.
Huddah ambaye hivi karibuni alidai kuwa Mustapha sio tabaka lake ‘not my class’, usiku wa jana aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akidai tabaka la wanaume anao-date nao wako busy wanataka kuingia kwenye orodha ya jarida la Forbes ambalo ni jarida maarufu zaidi duniani kwa kupanga viwango vya watu wenye mafanikio, na kuonesha kumshangaa Mustapha kwa kudai yeye yuko busy anatafuta umaarufu kwenye mitandao ya kijamii.
“The class of men I date are busy out there looking to be on Forbes list not busy looking for social media fame!!!!! Hehe! Never seen a man so bitter over a woman he only saw half naked a photo shoot….Chill, at least u got to take to floss with!” aliandika Huddah ambaye aliifuta post yake muda mfupi baadae.
Mustapha nae allimjibu kwa kejeli kuwa akapige picha na Bill Gates.
“I have moved on, I suggest she does the same,Next time, she should be wise n not leave photographic evidence! Ati anadate jamaa class ya forbes? haahahahahaha akapige picha na Bill Gates!" Amesema Mustapha.
Post A Comment: