Mamlaka
ya udhibiti wa safari za nchi kavu na majini (sumatra) imevitaka vyombo vyote vya usafiri hasa vya majini kuzingatia kanuni za ubabebaji wa
mizigo wakati wa safari.
Kauli
hiyo imekuja mara baada ya abiria watumiao usafiri wa meli kulalamikia vitendo
vya meli za kwenda bukoba kujaza mizigo kupita kiasi hali inayotishia usalama
wa safari zao.
Akizungumza
na afya radio afisa mfawidhi wa sumatra kanda
ya ziwa japhert ole loisumaye alisema
ubebaji wa mizigo unatazamwa kwa kupimwa na vifaa maalum na wala si kwa kukadilia
Akizungumzia tatizo la
kuchelewa kuondoka bandarini meli ya mv victoria loisumaye amesema wakati mwingine ni hali ya hewa ndio inachangiaMamlaka ya udhibiti wa nchi kavu na majini inawaomba wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo endapo wataona vyombo vya usafiri vinavunja kanuni na sheria za usafirishaji.
Post A Comment: