2014-05-04
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

 Siku chache baada ya kuandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini kufuatia kauli aliyoitoa  katika tuzo za Ktma msanii wa filamu Wema Sepetu ameendelea kusisitiza kuwa ile kauli ilitoka moyoni na alikusudia iwe hivyo. Wema kupitia ukurasa wake wake wa Intagram ameandika maelezo yanayoashiria kuwa haikuwa bahati mbaya au kwa sasabu tu furaha ilizidi akajikuta ameongea "Award zetu wenyewe za kila siku Tuna Award ya Monday mpaka sunday...eti...hihihihihihi so my Darling mi naweka tu picha kuna ambazo sijatumiwa ..ndo I'm waiting nizipate then nizipost okay...kama show ya Mtwara na nyingine za hapa I guess...okay" aliandika Wema akiwa ameambatanisha na picha inayomuonesha akiwa na mwenzi wake huyo huku wamezikumbatia tuzo hizo.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Proffesor Jay akiwa na Jose Chamelleon
Mmiliki wa studio ya Mwanalizombe amabaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Joseph Haule ama Professor Jay yuko mbion kuachia kazi mpya aliyofanya na msanii kutoka nchini Uganda Jose Chamelleon anayetamba na kibao chake cha Tubonge.Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyu amepost picha zinazomuonesha akiwa studio na msanii huyo wa uganda sambamba na Producer wake akiwa ameambatanisha na maelezo yanayoashiria kuna wimbo mpya wanaurekodi katika studio hiyo.







s

J
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii Keisha mara baada ya kujifungua
Siku chache baada ya kujifungua msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyetamba na nyimbo zake za nimechoka,nakuonea huruma,uvumilivu na nyingine nyingi aitwaye Keysha ameeleza hadi hivi sasa anazidi kuimarika kiafya pia mwanae anaendelea vizuri.Msanii huyo alijifungua mtoto wa kiume mapema juma tatu ya tarehe 5may 2014 katika hospitali ya Mount Mkobozi Kinondoni jijini Dar es salam na kufikisha idadi ya watoto wawili.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Rayc akiwa hospitali

Taarifa kutoka katika ukurasa wa face book wa xxl clouds fm msanii wa muziki hapa nchini
 Rehema chalamila ama Rayc amelazwa katika hospitali ya mwananyamala jijini Dar akisumbuliwa na ugonjwa wa dengue.  Taarifa hiyo isiyokuwa na maelezo zaidi imeambatanishwa pamoja na picha inayomuonesha msanii huyo akiwa amelala katika kitanda cha hospitali. Bongo20 inendelea kufuatilia ili kujua kinachoendelea
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Muandishi wa Afya radio Harith Jaha akizungumza na mkazi wa Kisesa katika kisima wanachorumia kuteka maji




Muandishi wa Afya radio Iddi Juma akifanya mahojiano na mkazi wa kisesa



Baadhi ya wakazi wa mji wa Kisesa wilaya ya magu mkoani Mwanza wapo hatarini kupatwa na magonjwa yanayotokana na utumiaji wa maji yasiyo salama.Wakizungumza na kipindi cha Kurunzi cha Afya radio Mwanza walisema wanalazimika kutumia maji hayo kutokana uhaba wa maji unaowakabili. Waliongeza kuwa mji huo umekuwa akikabiliwa na uhaba wa maji ambapo tegemeo lao kubwa ni visima ambavyo kuna wakati navyo hukauka na kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi. "Mabomba yapo lakini ni machache na pia yanatoa maji kidogo na kwa muda mfupi yani unaweza kuja saa kumi na mbili asubui ukatoka saa saba mchana na wakati mwingine adi saa kumi kutokana na foleni ya ndoo" Alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.Kufuatia kero hiyo kipindi hicho kilimtafuta afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini mwanza Bw.Robert Masunya ambaye alikiri kujua tatizo hilo na kuwaomba wakazi hao kuwa wavumilivu kwa kuwa tayari mpango wa kupeleka maji eneo hilo umekwishaa na tayari wamekwisha tandaza bomba hadi katika eneo la Kanyama kuelekea Kisesa.Kwa ujumla wakazi wa mtaa wa Kisesa wana hali ngumu katika huduma ya maji kutokana na upungufu wa mabomba pia uchakavu wa miundombinu ya mabomba na hata visima visivyokuwa salama.




Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Fid Q (katikati)Young Killer(kushoto) na Adamu Mchomvu(kulia)

Wasanii kutoka jijini Mwanza Fid Q na Young Killer wameweza kuweka muendelezo wa kuliweka jiji la mwanza katika ubora wa muziki baada ya kuchukua tuzo za Kilimanjaro music Awads.
Hii inakuja ikiwa ni baada ya mwaka jana jiji hilo kuwakilishwa vizuri na msanii Kala Jeremiah ambaye aliibuka na tuzo tatu.
Msanii Fid q amechukua tuzo za msanii bora wa Hiphop na mtunzi bora wa mwaka(hiphop) wakati young Killer akichukua tuzo ya msanii chipukizi.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Diamond na Ommy Dimpozi.(Picha na bongo5)
Diamond avunja rekodi iliyowahi kuwekwa na 20 percent kwa kuchukua tuzo saba.
Tazama  hapo chini majina ya washindi wa tuzo hizo


1. Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya tanzania - bora mchawi, dar bongo massive

2. Msanii bora chipukizi anayeibuka - young killer

3. Wimbo bora wa zouk - yahaya, lady jaydee

4. Wimbo bora wa afro pop - number one, diamond platnumz

5. Wimbo bora wa ragga / dancehall - nishai chibwa ft juru

6. Wimbo bora wa raggae - niwe na wewe, dabo

7.wimbo bora wa taarab - wasiwasi wako, mzee yusuf
8. Kikundi cha mwaka cha taarab - jahazi modern taarab

9. Mwimbaji bora wa kike taarab - isha ramadhani

10. Mwimbaji bora wa kiume taarab - mzee yusuf

11. Wimbo bora wa kiswahili bendi - ushamba mzigo, mashujaa band

12. Mwimbaji bora wa kike bendi - luiza mbutu

13. Mwimbaji bora wa kiume bendi - jose mara

14. Rapa bora wa mwaka bendi - furguson

15. Bendi ya mwaka - mashujaa band

16. Mwimbaji bora wa kike, kizazi kipya - lady jaydee

17. Mwimbaji bora wa kiume, kizazi kipya - diamond

18. Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya - weusi

19. Wimbo bora wa rnb - closer, vanessa mdee

20. Wimbo bora wa hip hop - nje ya box, nick wa pili ft joh makini & gnako

21. Msanii bora wa hip hop - fid q

22. Wimbo bora wa kushirikisha / kushirikiana - muziki gani, nay wa mitego ft diamond

23. Wimbo bora wa afrika mashariki - tubonge, jose chameleone

24. Mtunzi bora wa mwaka taarab - mzee yusuf

25. Mtunzi bora wa mwaka bendi - christian bella

26. Mtunzi bora wa mwaka kizazi kipya - diamond

27. Mtunzi bora wa mwaka hip hop - fid q

28. Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, taarab - enrico

29. Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, bendi - amoroso

30. Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka, kizazi kipya - man water, combination sound

31. Hall of fame, individual - hassan bitchuka

32. Hall of fame, institution - masoud masoud

33. Video bora ya muziki ya mwaka - number one, diamond

34.wimbo wa mwaka - number one. Diamond

35. Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki - isha ramadhani

36. Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki - diamond