2013-06-16
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

MSANII BARNABA AONDOKEWA NA MAMA YAKE




Msanii  Banaba Elias  maarafu kama Barnaba kutokaTanzania House of Talent (THT) amepatwa na msiba wa kuondokea na mama yake.
Habari zinasema msiba huo umetokea alfajiri ya leo nyumbani kwa mama yake Dar es salam ambapo mama yake huyo   imeripotiwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya presha.

Rafiki wa karibu wa msanii huyo aitwaye Amini amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

Habari zaidi kuhusu mazishi tutaendelea kukufahamisha kadiri tutakavyokuwa tukipata taarifa.
Inna lillah wa inna ilaih raajiuun. Mola ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Aamin!!
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
ZOEZI LA UOKOAJI WA NDEGE 

LILILOTIKISA JIJINI MWANZA



Ambulance ya waokoaji wakiwa Airport Mwanza  na baadhi ya askari


Leo baadhi ya wanachi jijini Mwanza wamejikuta katika wasiwasi mkubwa baada ya kupata taarifa kuwa kuna ndege imeanguka ziwani jijini humo na ilikuwa ikitokea Bujumbura na ilikuwa na abiria 50.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika toka uongozi wa juu zinasema hakuna ajali yoyote iliyotokea isipokuwa kulikuwa na zoezi la uokoaji wa ajali za ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza likiwa na lengo la kupima utayari wa idara za uokoaji kama vile hospitali, jeshi la zimamoto, jeshi la polisi na wananchi kwa ujumla.

mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha mwanza  Ester Madare amesema katika zoezi hilo walikuwa wakiangalia vyombo hivyo vitafika wakati gani na madhara kiasi gani yanaweza kutokea.

Amesema ndege iliyoandaliwa ilikuwa na abiria hamsini walioandaliwa na wote wakiwa na ujuzi wa kuogelea huku mmoja kati yao aliigiza amefariki na zoezi lilianza saa nne na dakika 17 asubuhi na na kumalizika saa sita mchana.

Nao baadhi ya mashuhuda wa zoezi hilo ambao pia wameshiriki katika uokoaji wamesema zoezi hilo limeenda vizuri na idara zote za uokoaji zimejitahidi kuwahi kutoa huduma.

Mashuhuda wengine wametoa kasoro baadhi ya idara zilizo na boti ziendazo kasi kwa kutofika kwa wakati lakini pia umeonekana upungufu wa  boti hizo.

Mpaka waandishi wa Afya radio Mwanza IDDI JUMA NA NOEL THOMPSON  wanaondoka uwanjani hapo tathimini ya utendaji wa zoezi kwa  idara husika ilikuwa bado haijafanyika na meneja wa uwanja huo amesema tathimini hiyo itatolewa pindi itakapokamilika.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

KAKA WA KIM KARDASHIAN ASEMA

HAHITAJI KUJUA JINA LA MTOTO WA

DADA YAKE

Kaka wa mzazi mwenza wa msanii Kanye west anayetambulika kwa jina la Brody Jenner amesema kwa sasa haoni umuhimu wa yeye kufahamu jina la mtoto wa dada yake anayeitwa Kim Kardashian.

Akizungumza katika interview  na kituo kimoja cha radio, Jenner amesema hadi sasa hajui jina la mtoto huyo na kuongeza kuna mambo mengi  ya kufanya na muhimu zaidi ya hilo.

Ameongeza hadi sasa bado hajamuona mtoto huyo na kuwa hajawa na uharaka wa kumuona ila siku akipata tym atamuona .

Tangu kuzaliwa kwa mtoto huyo kumekuwa na usiri unaofanywa na wazazi wake juu ya kutoa taarifa mbalimbali za mtoto huyo.

Hata hivyo kuna baadhi ya mitandao iliyoripoti kuwa jina la mtoto huyo tayari limekwisha fahamika na anaitwa North East japo wao bado hawajasikika rasmi wakielezea jina hilo.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Baada ya kuwepo kwa shauku ya mashabiki wa muziki katika nchi mbali mbali dunian ya kutaka kujua jina la mtoto wa Kanye west na kim kardashian  kunataarifa zimetoka zinazoweka wazi jina la kichanga hicho.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

MANDOJO NA DOMO KAYA

WAFUNGUKA KILICHOWAFANYA

KUWAKIMYA MUDA MREFU


Wasanii wa bongo fleva Mandojo na domo kaya waliowahi kutamba na ngoma kama nikupe, niaje, na nyingine kibao wameelezea sababu za kimya chao.

Akizungumza na muandishi wetu mmoja wa wasanii hao Mandojo amesema ukimya wao ulitokana na mambo yao yakibiashara ambayo yaliwaweka mbali kidogo na muziki na ndo maana wakawa kimya.

Hata hivyo ameeleza hivi sasa tayari mipango yao ya kurudi kwenye gemu imekwisha kamilika na hivi karibuni wataachia ngoma.

Mandojo amesema ujio wao sio wa kubahatisha kwani wameisoma gemu muda mrefu na wanatarajia kuja na syle yao ileile ya mwanzo na  safari hii wakiiboresha zaidi.

“ tumejipanga vizuri na tunatarajia mashabiki wetu watapata walichokikosa toka kwetu na safari hii tunakuja kiutu uzima sio kama kina mandojo na domo kaya wa kipindi kile”  alisema Mandojo


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

MASHIRIKA NA WANAHARAKATI

WAMPONDA KANYE WEST

Mashirika mbali mbali na wanaharakati wanaofnya juhudi za kupambana na ugonjwa wa kutikisika mwili uitwao “ PARKINSON”  wamelaani kitendo cha msanii Kanye west kuandika mashairi yanayoonesha kuukejeli ugonjwa huo kupitia wimbo wake wa ON SIGHT.

Mashairi hayo yanayosema “ soon as I pull up and park the benz, we get bitch shaking like parkinson’s” yametafisiriwa kwa mtazamo tofauti na wanaharakati hao na kudai kuwa wakati wao wanafanya juhudi za kupambana nao, Kanye anaonesha kuupuuza.

Moja kati ya mashirika hayo la Parkinson’s UK la nchini uingereza limesema Kanye ameonesha ukatili na upumbavu kwa waathirika wa ugonjwa huo.

Kwa upande wa wanaharakati kutoka nchini New Zealand wao wamesema wakati wao wakiendelea kuoa elimu juu ya ugonjwa huo na kuonesha dalili za mafanikio,wamejikuta wakipatwa na masikitiko baada ya kushuhudia ukosefu wa huruma toka kwenye mistari hiyo ya Kanye.

Kwa upande wa Marekani wamechukulia mashairi hayo kama ujinga na yaliyokosa staha ama heshima


Ugonjwa huu umetajwa kusumbua watu wengi katika nchi mbali mbali duniani na husababishwa na matatizo yanayojitokeza kwenye ubongo na mmoja kati ya waathirika a ugonjwa huo ni Mohammad Ali mwanamasumbwi wa zamani.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

SAIDA KAROLI : SIJAFA MI NIKO HAI NA SALAMA


Baada ya kuwepo kwa uvumi  kuwa msanii Saida Karoli amefariki yeye aibuka na kukanusha uvumi huo.

Akizungumza na muandishi wetu msanii huyu amesema yeye yu hai na salama na yupo mkoani mbeya akiendelea na shughuli zake.

Saida amesema ameshangazwa na uvumi huo na kuwataka watanzania wajue kuwa yeye yu hai.

Mbali na hilo pia amewashukuru waandishi wa habari kwa kutoa ushirikiano katika kukanusha taarifa hizi.

Hapo jana kulizuka taarifa zilizodai kuwa saida karoli ameaga dunia baada ya kupata ajali ya boti akitokea visiwan kufanya show.



Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

BEN POL AONGEA BAADA YA KUINGIA KWENYE TUZO MPYA ZA  YOUTH FOR AFRICA UNDER 30 YEARS KWA 2013


Baadaya kuingizwa kwenye tuzo za youth for Africa katika kipengele cha burudani msanii Ben pol amesema hali hiyo inamfanya kuongeza bidii zaidi katika kazi zake.

Akizungumza na muandishi wetu leo hii msanii huyu amesema tuzo hizo zimemtia moyo zaidi na kuahidi kufanya vizuri zaidi kwa ajili ya mashabiki wake.

Licha ya kuwa bado hajajua kama tuzo hizo zitahitaji kura za mashabiki amewaomba mashabiki kukaa tayari kwa lolote kwa ajili ya kumsapoti na endapo ikitokea mshinidi atahitaji kura za watu basi wampigie.

Wasanii wengine walioingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Vanesa Mdee Lina na Michael Mlingwa.

Hivi karibuni msanii huyu amekuwa ni mmoja kati ya wasanii walioibuka na tuzo katika tuzo za Kilimanjaro music Award.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
DRAKE AONESHA NIA YA KUMALIZA BIFU NA CHRISS BROWN
Msanii Drake mzaliwa wa Canada anayeshika na wimbo wa start from the bottom ameamua kurudi nyuma na kutaka kukaa chini na Chriss brown kumaliza tofauti zao.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mtv Drake aliliambia jarida la GQ kuwa ana mpango huo ili warudi katika hali waliyokuwa nayo awali.

Habari zaidi zinasema Drake alisema kuwa hawezi kumzingua mtu hadi pale atakapo zinguliwa.

Aliongeza zaidi kuwa anahitaji kuelekeza nguvu zake kwenye albamu yake ijayo na sio bifu lisilo na manufaa kati yao.

Ugomvi wa mastaa hawa ulitokana na Chriss kumshutumu Drake kutembea na mpenzi wake wa zamani Rihana na itakumbukwa watu hawa wamewahi kufanyiana fujo katika club ya usiku huko new York Marekani.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

JOH MAKIN YUKO FITI NA ANAENDELEA NA MISHE KAMA KAWA

Hali ya msanii Joh Makin imeimarika na sasa yupo na anaendelea na shughuli zake.

Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu, mdogo wa msanii huyo Nick wa pili amesema Joh amepona na anendelea na mishe kama kawaida.

“yaah, ni kweli Joh alikuwa anaumwa lakini sasa hivi amekwishapona na anaendelea na mishemishe kama kawaida” alisema Nick.

Hivi karibuni kuliripotiwa kuwa msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya malaria hali iliyomfanya kulazwa katika hospitali moja huko Dar Es salam.



Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
MTOTO WA MICHAEL JACKSON ASEMA

ANAMCHUKIA JUSTINE BIEBER


Mtoto wa kike wa  aliyekuwa mwanamuziki na star duniani kote Michael Jackson,amesema anamchukia mwanamuziki justine bieber.

Kwa mujibu wa mtandao wa Tmz wa nchini Marekani msichana huyo anayejulikana kwa jina la Paris Jackson anamchukia Bieber kutokana na kutozungumza chochote juu ya wasichana walio tweet kujidhuru kwa kujikata visu wenyewe  kama ishara ya mapenzi kwake.

Binti huyo ameeleza kuwa Bieber ndiye roll model wa wasichana wengi wa kike  na anatakiwa kutumia nafasi hiyo kuwaondoa wasichana hao katika hali hiyo lakini badala yake amekuwa akitumia muda wake kuwaongela kwa mambo mengine.

Habari zaidi zinasema msichana huyo aliudhika zaidi baada ya kuziona picha zilizo postiwa na mtandao wa TMZ  zilizomuonesha Justine akivuta wida hotelin January mwaka huu.

Hivi karibuni msichana huyu alijaribu kujiondoa duniani kwa kutumia kisu kwa madai ya kumkumbuka sana baba yake na hakuna mtu anaemuonesha mapenzi kama aliyokuwa akipewa na baba yake.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

AFANDE SELE :

MUZIKIUNAKUA,WASANII WANASHUKA


Msanii wa bongo fleva aliyewahi kuwa mfalme wa Rhymes hapa bongo Suleiman Msindi au Afande sele amesema wakati muziki wa bongo ukipanda wasanii wa muziki huo wanashuka.

Msanii huyu amesema kiwango cha muziki nchini kinazidi kukuwa kwa maana ya kupata nafasi zaidi katika jamii ukilinganisha na mwanzo wakati muziki huo ukionekana wa kihuni.

Ameongeza hivi sasa wasanii wanapata nafasi ya kufanya kazi na wasanii wa nje na kupata mafaniko ukilinganisha na mwanzo ambapo wasanii walilipwa pesa kidogo na hawakuwa wakifahamika sana nje.

Ameeleza tatizo lililopo katika muziki huu kwa sasa ni kuwa wasanii wanashuka kiuandishi kwa maana ya kuandika mashairi mepesi ukilinganisha na nyuma ambapo walitumia akilizaidi katika uandishi wa nyimbo zao.

Msanii huyu amewahi kutamba na nyimbo kama Darubini,Watu na pesa Acha kupiga mayowe na nyingine nyingi na ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wanaoheshimika kwa utunzi na uandishi wa mashairi.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
SAJNA: NEY WA MITEGO ANAUFAHAMU

WIMBO WA  "MPIRA GANI"



Msanii wa Bongofleva Sajna aliyewahi kutamba na nyimbo kama Iveta sitaki kuumizwa na nyingine nyingi amesema wimbo wa MPIRA GANI aliyotumia style na melody ya wimbo wa Muziki gani,mmiliki wake anaufahamu.

Akizungumza mwishoni mwa wiki hii msanii huyu alisema kabla ya kuufanya  wimbo huo alimtaarifu Ney ambaye ndiye mmiliki na kuruhusiwa kuufanya kwa ajili ya mashabiki.

Amesema watu wamekuwa wakidhani kuwa alikurupuka bila kutoa taarifa na hivyo amewaomba waelewe hivyo na endapo kukitokea hawataamini ni ruksa kumtafuta Ney na kumuuliza.

Akizungumzia kwanini ameamua kutumia style na melody ya wimbo huo amesema ilitokana na mapendekezo yaliyotolewa na watu wake wa karibu ambao walimshauri afanye hivyo kama zawadi kwa mashabiki na haikuwa kwa ajili ya kuuachia kama ilivyo sasa.

Sajna amesema hivi karibuni anatarajia kuachia rasmi ngoma mpya ambayo ilipangwa kutoka kabla ya MPIRA GANI

“kuna wimbo ambao natarajia kuuachia hivi karibuni nimewashirikisha Ben Pol na C- sir Madin kwa hiyo mashabiki wakae yatari kunipokea” alisema Sajna.