MANDOJO NA DOMO KAYA
WAFUNGUKA KILICHOWAFANYA
KUWAKIMYA MUDA MREFU
Wasanii wa bongo fleva Mandojo na domo kaya waliowahi
kutamba na ngoma kama nikupe, niaje, na nyingine kibao wameelezea sababu za
kimya chao.
Akizungumza na muandishi wetu mmoja wa wasanii hao
Mandojo amesema ukimya wao ulitokana na mambo yao yakibiashara ambayo
yaliwaweka mbali kidogo na muziki na ndo maana wakawa kimya.
Hata hivyo ameeleza hivi sasa tayari mipango yao ya
kurudi kwenye gemu imekwisha kamilika na hivi karibuni wataachia ngoma.
Mandojo amesema ujio wao sio wa kubahatisha kwani
wameisoma gemu muda mrefu na wanatarajia kuja na syle yao ileile ya mwanzo na safari hii wakiiboresha zaidi.
“ tumejipanga vizuri na tunatarajia mashabiki wetu
watapata walichokikosa toka kwetu na safari hii tunakuja kiutu uzima sio kama
kina mandojo na domo kaya wa kipindi kile” alisema Mandojo
Post A Comment: