MASHIRIKA
NA WANAHARAKATI
WAMPONDA KANYE WEST
Mashirika mbali mbali
na wanaharakati wanaofnya juhudi za kupambana na ugonjwa wa kutikisika mwili uitwao
“ PARKINSON” wamelaani kitendo cha
msanii Kanye west kuandika mashairi yanayoonesha kuukejeli ugonjwa huo kupitia
wimbo wake wa ON SIGHT.
Mashairi hayo
yanayosema “ soon as I pull up and park the benz, we get bitch shaking like parkinson’s”
yametafisiriwa kwa mtazamo tofauti na wanaharakati hao na kudai kuwa wakati wao
wanafanya juhudi za kupambana nao, Kanye anaonesha kuupuuza.
Moja kati ya mashirika
hayo la Parkinson’s UK la nchini uingereza limesema Kanye ameonesha ukatili na upumbavu
kwa waathirika wa ugonjwa huo.
Kwa upande wa
wanaharakati kutoka nchini New Zealand wao wamesema wakati wao wakiendelea kuoa
elimu juu ya ugonjwa huo na kuonesha dalili za mafanikio,wamejikuta wakipatwa
na masikitiko baada ya kushuhudia ukosefu wa huruma toka kwenye mistari hiyo ya
Kanye.
Kwa upande wa Marekani
wamechukulia mashairi hayo kama ujinga na yaliyokosa staha ama heshima
Ugonjwa huu umetajwa
kusumbua watu wengi katika nchi mbali mbali duniani na husababishwa na matatizo
yanayojitokeza kwenye ubongo na mmoja kati ya waathirika a ugonjwa huo ni
Mohammad Ali mwanamasumbwi wa zamani.
Post A Comment: