SAIDA KAROLI : SIJAFA MI NIKO HAI NA SALAMA


Baada ya kuwepo kwa uvumi  kuwa msanii Saida Karoli amefariki yeye aibuka na kukanusha uvumi huo.

Akizungumza na muandishi wetu msanii huyu amesema yeye yu hai na salama na yupo mkoani mbeya akiendelea na shughuli zake.

Saida amesema ameshangazwa na uvumi huo na kuwataka watanzania wajue kuwa yeye yu hai.

Mbali na hilo pia amewashukuru waandishi wa habari kwa kutoa ushirikiano katika kukanusha taarifa hizi.

Hapo jana kulizuka taarifa zilizodai kuwa saida karoli ameaga dunia baada ya kupata ajali ya boti akitokea visiwan kufanya show.



Axact

Post A Comment: