2015-07-12
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Ni simulizi kali na ya kusisimua ambayo ndani yake kuna furaha majonzi hasira visasi na mengine mengi.inayomuhusu msichana Betha aliyezaliwa katika maisha ya kifahari na baadaye kugeuka ombaomba baada ya wazazi wake kupoteza maisha. alipitia misukosuko sana ikiwemo kubakwa na baba yake mdogo na vijana wengine mitaani alikokuwa akilala na kuishi kutokna na kukosa mahala pa kuishi.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Takriban wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka.

Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka kwa vifusi vya jengo hilo.

Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa ameileza runinga ya Urusi kwamba wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali hiyo.

Picha za televisheni zilionyesha sehemu ya jengo hilo la ghorofa nne likiwa limeharibika kabisa huku wanajeshi wakishirikiana kuondosha vifusi.

Mwandishi wa BBC Moscow amesema inadhaniwa kwamba ukarabati duni uliofanyika mwaka jana ndio uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Baadhi ya wananchi wa mtaa wa S.D.A uliopo kata ya isamilo jijini mwanza wamesema wako njia panda kutokana na kutojua sababu za kujiuzuru kwa mwenyekiti wa mtaa huo.

Wananchi hao wamesema hali hiyo imewaathiri kutokana na kumtegemea kwa kiasi kikubwa katika shughuli za mtaa wao.

Wameongeza ni vyema angeweka wazi jambo lililomfanya kuachia madaraka hayo .

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa mtaa huo amesema sababu kubwa iliyomfanya kuachia madaraka ni kutokana na kuhama makazi na kupata ajira katika eneo jingine.

Kukosekana kwa wenyeviti wa mitaa katika baadhi ya maeneo kumeelzwa kurudisha nyuma maendleo ya mitaa hiyo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Maafisa wanne wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam Tanzania.
Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam.
Polisi wanasema kuwa wavamizi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.
Waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Kwa mujibu na raia wanoishi karibu na kituo hicho,makabiliano ya risasi yalidumu kwa zaidi ya saa moja.

Mkuu wa polisi Ernest Mangu amethibitisha uvamizi huo akisema askari 4 na raia 3 wameaga dunia.
Hadi sasa haijabainika iwapo kuna majeruhi.
Aidha amesema kuwa walipora handaki ya kituo hicho na kuiba bunduki za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana.

Hakuna aliyekamatwa kufuatia shambulizi hilo japo maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi.
Kulikuwa na matone ya damu nje ya kituo hicho cha polisi dalili kuwa waliojeruhiwa walikuwa wakijaribu kutafuta msaada.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo japo bwana Mangu anasema kuwa ni mapema mno kusema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kigaidi.
Hii si mara ya kwanza kwa kituo cha polisi kuvamiwa, mwaka uliopita kundi la watu waliokuwa wamejihami lilivamia kituo cha polisi na kukimbilia mwituni.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Kuingia kwa simu za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kuchukua picha nchin maarufu kama smart phone kumetajwa kuathiri soko la vijana wanaojishughulisha na upigaji wa picha.

Baadhi ya vijana wanaopiga picha katika mzunguko wa samaki jijini mwanza wakizungumza na muandishi weut walisema hali imekuwa tofauti na mwanzo kabla simu hizo hazijaingia.

Walieleza hivi sasa watu wengi wamekuwa wazito kupiga picha kama ilivyokuwa awali jambo linaloleta changamoto kubwa katika ajira yao.

Mbali na hivyo wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwaendeleza vijana kwa kuwapa maeneo na mikopo kwa ajili ya biashara.

Kukua kwa teknolojia kumeendelea kupunguza ajira katika sekta mbalimbali licha ya kurahisisha huduma mbalimbali zikiwemo za mawasiliano na hata za kulipia umeme.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)





Walimu wa kuu wa shule za msingi mkoani geita wametakiwa kutoa taarifa za walimu wanaoacha kufundisha na kuendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda wakati wa masomo.
Habari kutoka mkoani humo zinasema walimu wa shule za msingi wamekuwa wakiacha kufundisha watoto na badala yake kwenda kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kuendesha pikipiki hizo.

 Afisa elimu mkoa wa geita efrancia bachuma amsema hali hiyo haikubaliki na kuwa walimu wakuu watoe taarifa ili walimu hao wachukulie hatua za kinidhamu.

 Ameongeza vitedo hivyo vinawaathiri wananfunzi kwa kuwa hawapati masomo kama inavyostahili.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wamesema hali hiyo imewafanya kushindwa kufaulu katika masomo yao.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Mteuliwa wa chama cha mapinduzi katika mbio za kuwania kiti ch uraisi katika uchaguzi mkuu mwaka huu waziri john magufuli amesema atahakikisha analeta maendeleo kwa wananchi wote bila kujali itikadi endapo atapita katika kiti hicho.

Katika mkutano wa kumtangaza rasmi kiongozi huyo huyo amesema licha ya kuwa taifa lina wananchi kutoka vyama tofauti atahakikisha ana boresha maisha kwa kila mwananchi

Magufuli alisema hayo katka mkutano uliofanyika katika uwanja wa jamhuri mjin dodoma.

Wakati huo huo kuna taarifa zina sema muungano wa vyama vya umoja wa katiba ukawa umesema hautishwi na uteuzi wa magufuli.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Baadhi ya wajumbe wa umoja wa vijana wilaya ya nyamagana mkoani mwanza wamemtaka mwenyekiti wa umja huo hussein kimu kuuomba radhi umoja huo kutokana na taarifa yake kwa vyombo vya habari ikisema umoja huo unamtuhumu kiongozi edward lowasa kuandaa vijana kwa ajili ya kufanya fujo mjin dodoma.
Mmja wa wajumbe hao omari juma yahya ambaye ni mwenyekiti wa vijana kata ya mirongo amesema wao hawahusiki na kauli hiyo na kuwa anapaswa kuomba radhi.
Ameongeza kinyume na hivyo huenda wajumbe hao wakafanya maamuzi magumu.
Naye mjumbe mwingine kutoka katika umoja huo amesema mbali na kuomba radhi anapaswa kufuta kauli aliyoitoa kwa vyombo vya habari sambamba na kushughlikia maswala yanayohusu umja huo.

Mapema wiki iliyopita mwenyekiti wa umoja huo hussein kimu alimshutumu aliyekuwa mtia nia wa kuwania mbio za uraisi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm edward lowasa kuwa alifanya mpango wa kuandaa vijana wakiwemo mabaunsa ili kufanya vurugu Dodoma endapo jina lake litakatwa.
Bongo 20 na Jembe habari vinaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Hussein kimu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm ili kuzungumzia shutuma hizo.