Kuingia kwa simu za
kisasa zenye uwezo mkubwa wa kuchukua picha nchin maarufu kama smart phone kumetajwa kuathiri soko la
vijana wanaojishughulisha na upigaji wa picha.
Baadhi ya vijana wanaopiga picha katika mzunguko wa samaki jijini mwanza
wakizungumza na muandishi weut walisema hali imekuwa tofauti na mwanzo kabla simu hizo hazijaingia.
Walieleza hivi sasa
watu wengi wamekuwa wazito kupiga picha kama ilivyokuwa awali jambo linaloleta
changamoto kubwa katika ajira yao.
Mbali na hivyo
wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwaendeleza vijana kwa kuwapa maeneo na
mikopo kwa ajili ya biashara.
Kukua kwa teknolojia
kumeendelea kupunguza ajira katika sekta mbalimbali licha ya kurahisisha huduma
mbalimbali zikiwemo za mawasiliano na hata za kulipia umeme.
Post A Comment: