2013-06-30
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

 Ney akiwa ndani ya studio za Afya Radio
Siku chache Baada ya kufanyika kwa show iliyoleta madhara kwa baadhi ya mashabiki jijin Mwanza Msanii Ney wa mitego ametoa pole kwa mashabiki hao.
Kupitia show ya Extra Vaganza ya Afya radio Mwanza msanii huyu amesema kilichotokea hakikuwa kimepangwa na mtu yeyote na kuwa ilitokea kama bahati mbaya tu na kuwa wao lengo lao ilikuwa ni kutoa burudani tu kwa mashabiki wao.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
WOLPER: HATA KAMA HALIMA MDEE AMETOKA JESHINI NITAMCHAPA TU
 
Jackline Wolper
 

Zikiwa zimebaki siku chache kufikia tamasha la Matumaini ambalo litahusisha wasanii mbali mbali na viongozi hapa nchini katika michezo mbali mbali, msanii Jackline Wolper amesema atamgaragaza mpizani wake Mh. mbunge Halima Mdee.

Akifunguka leo hii msanii huyu amesema licha ya kuwa mpinzani wake amepitia mafunzo ya kijeshi lakini yeye haangalii hilo kwani bado sio kigezo cha kumtisha na kuwa yeye yuko fiti na atahakikisha anapata ushindi.

Wolper amesema Halima ni mtu wa siasa na kuongea sana na yeye ni mtu wa kuigiza na vitendo hivyo siku hiyo kazi yake kubwa itakuwa ni moja tu ya kumtandika na sio maneno.

Pambano jingine la masumbwi linalotarajiwa kufanyika ni la Vicent Kigosi maarufu kama Ray dhidi ya Mh. mbunge Zitto Zuberi Kabwe.

Tamasha la matumaini linatarajiwa kufanyika tarehe 7 July2013 katika uwanja wa mpira wa miguu wa taifa.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

ALIYEJIFANYA JOKATE AKAMATWA

Mpeka,kijana anayedaiwa kutumia jina la Jokate
 
 
Mwanaume mmoja aliyekuwa akitumia jina la Jokate katika mitandao ya kijamii na simu kuwasiliana na watu amekamatwa na polisi jijini Dar es salam.
 
Habari zinasema mtu huyo alikamatwa baada ya kutangaza kuwa Kidoti hair na Mzinga Planet wanahitaji mamodo kwa ajili ya kutengeneza matangazo kwa ajili ya nywele za kidoti.
 
Baada ya taarifa hizo msichana mmoja aliyewahi kushiriki miss morogoro 2003 (jina tunalo ) aliwasili katika mzalendo pub kama taarifa zilivyokuwa zikieleza tayari kwa usaili.
 
Cha ajabu dada huyo alipofika hapo hakukuta mtu na kuamua kumpigia mtu wa karibu wa Jokate aliyefahamika kwa jina moja la  Johnson ambaye alionesha kushangazwa na taarifa hiyo na kuamua kumtafuta Jokate mwenyewe ambaye alifika muda mfupi baadae.
 
Imeelezwa baada ya kuwasili waliwakuta majaji wa usaili huo ambao walisema hawajui chochote juu ya kutumiwa jina la kidoti bila ruhusa na ndipo walipomtafuta muhusika aliyefahamika kwa jina moja la Mpeka ambaye aliwasili eneo hilo na kuonesha kujikanyaga pindi alipoulizwa juu ya swala hilo
 
Baada ya muda kidogo Jokate na wenzie waliamua kuwaita polisi ambao walimtia mbaroni kijana huyo kwa ajili ya kufanya nae mahojiano juu ya kitendo alichofanya.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

MAJANGA ILINIPA DILI SOUTH AFRIKA



Msanii wa muziki na filamu hapa nchini Snura Mushi maarufu kama Snura amesema wimbo wa majanga ulimpa dili la kufanya filamu nchini Afrika kusini.

Akifunguka hivi karibuni msanii huyu amesema dili hilo lilikuja mara baada ya waandaaji wa filamu mpya inaayoitwa Tandeka nchini humo kumuona akishoot video ya wimbo wake huo wa Majanga na kuvutiwa naye.

Ameeleza baada ya hapo walimtafuta na kumuita kwenye usahili na baada ya kufaulu walimpa nafasi ya muhusika mkuu.

Imeelezwa kuwa filamu hiyo imetumia lugha mbalimbali zikiwemo Kiswahili, Kizulu na Kiingereza.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO KATIKA BONANZA LA AFYA RADIO MWANZA NA KITUO CHA SOKA CHA ALLIANCE


HARITH JAHA(MR CREDIT) KATIKA SHINDANO LA KUNYWA SODA

KIOSI CHA AFYA RADIO

MMOJA KATI YA WATANGAZAJI WA MECHI HIYO

WACHEZAJI WA AFYA RADIO NOUR (KULIA)NA NOEL(KUSHOTO)

BAADHI YA WADADA WA AFYA RADIO,SANZA(KUSHOTO) CLARA(KULIA)

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

CP: PARKLANE IMEKWISHA RUDI



Baada ya miaka kadhaa kupita kukiwa na ukimya kwa kundi la Park lane hivi sasa imeripotiwa kundi hilo lililounganisha wasanii wa wawili Sumalee na CP limerejea tena.

Kwa mujibu wa msanii mmoja kati ya wanaounganisha kundi hilo Ilunga Khalifa au CP kundi hilo lip na tayari kuna nyimbo mbili zimeshafanywa na mmoja wapo  unatarajiwa kuachiwa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 Kundi hili la Parklane liliwahi kutamba enzi za nyuma na nyimbo kama Aisha,Nafasi nyingine kabla ya kila mmoja kuamua kufanya kama solo artist.