ALIYEJIFANYA JOKATE AKAMATWA
Mpeka,kijana anayedaiwa kutumia jina la Jokate
Mwanaume mmoja
aliyekuwa akitumia jina la Jokate katika mitandao ya kijamii na simu
kuwasiliana na watu amekamatwa na polisi jijini Dar es salam.
Habari zinasema mtu
huyo alikamatwa baada ya kutangaza kuwa Kidoti hair
na Mzinga Planet wanahitaji mamodo kwa ajili ya kutengeneza matangazo kwa ajili
ya nywele za kidoti.
Baada ya taarifa hizo
msichana mmoja aliyewahi kushiriki miss morogoro 2003 (jina tunalo ) aliwasili
katika mzalendo pub kama taarifa zilivyokuwa zikieleza tayari kwa usaili.
Cha ajabu dada huyo
alipofika hapo hakukuta mtu na kuamua kumpigia mtu wa karibu wa Jokate aliyefahamika kwa jina moja la Johnson ambaye alionesha kushangazwa na
taarifa hiyo na kuamua kumtafuta Jokate mwenyewe ambaye alifika muda mfupi
baadae.
Imeelezwa baada ya
kuwasili waliwakuta majaji wa usaili huo ambao walisema hawajui chochote juu ya
kutumiwa jina la kidoti bila ruhusa na ndipo walipomtafuta muhusika aliyefahamika
kwa jina moja la Mpeka ambaye aliwasili eneo hilo na kuonesha kujikanyaga pindi
alipoulizwa juu ya swala hilo
Baada ya muda kidogo
Jokate na wenzie waliamua kuwaita polisi ambao walimtia mbaroni kijana huyo kwa
ajili ya kufanya nae mahojiano juu ya kitendo alichofanya.
Post A Comment: