WOLPER: HATA KAMA HALIMA MDEE AMETOKA JESHINI NITAMCHAPA TU
 
Jackline Wolper
 

Zikiwa zimebaki siku chache kufikia tamasha la Matumaini ambalo litahusisha wasanii mbali mbali na viongozi hapa nchini katika michezo mbali mbali, msanii Jackline Wolper amesema atamgaragaza mpizani wake Mh. mbunge Halima Mdee.

Akifunguka leo hii msanii huyu amesema licha ya kuwa mpinzani wake amepitia mafunzo ya kijeshi lakini yeye haangalii hilo kwani bado sio kigezo cha kumtisha na kuwa yeye yuko fiti na atahakikisha anapata ushindi.

Wolper amesema Halima ni mtu wa siasa na kuongea sana na yeye ni mtu wa kuigiza na vitendo hivyo siku hiyo kazi yake kubwa itakuwa ni moja tu ya kumtandika na sio maneno.

Pambano jingine la masumbwi linalotarajiwa kufanyika ni la Vicent Kigosi maarufu kama Ray dhidi ya Mh. mbunge Zitto Zuberi Kabwe.

Tamasha la matumaini linatarajiwa kufanyika tarehe 7 July2013 katika uwanja wa mpira wa miguu wa taifa.
Axact

Post A Comment: