Ney akiwa ndani ya studio za Afya Radio
Kupitia show ya Extra Vaganza ya Afya radio Mwanza msanii huyu amesema kilichotokea hakikuwa kimepangwa na mtu yeyote na kuwa ilitokea kama bahati mbaya tu na kuwa wao lengo lao ilikuwa ni kutoa burudani tu kwa mashabiki wao.
Amesema japo lilikuwa ni jambo zito hasa kwa waliopata madhara lakini mashabiki wanapaswa kuulia na kuchukulia kama ni sehemu ya maisha na kuwa imetokea kama ajali nyingine zinavyoweza kutokea.
Jumapili ya tareh30June 2013 katika uwanja wa ccm kirumba jiji Mwanza kulifanyika show kubwa iliyokutanisha wasanii mbalimbali wa Bongo fleva na iliandaliwa na mtandao wa Tigo, haata hivyo sho hiyo haikufika mwisho kutokana na vurugu zilizotokea.
Ney wa Mitego akiwa jukwaani |
Vurugu hizo zlitokea mara baada ya msanii Diamond kuwaambia mashabiki waogee karibu na jukwaa ili awape burudani kwa ukaribu zaidi , kauli hiyo ilizua tafrani mara baada ya watu waliokuwa wamefika kwa uwingi sana kusogea na kupoteza utulivu hali iliyowalazimu askari wa jeshi la polisi na mabaunsa kufanya kazi ya ziada kuondoa hali hiyo na kukatisha show na kumtoa msanii huyo ndani ya uwanja kwa ulinzi.
Post A Comment: