Ray C                                                                                                  Rachel

Wasanii wa kizazi kipya hapa nchini Rehema Charamila  au Rayc na msanii mwingine aitwae Recho au Miss upepo huenda wakakutana na kurekodi wimbo.
Hatua hii imekuja kufuatia majibu aliyoyatoa Msanii Rayc kwa mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kuulizwa anamchukuliaje Recho.

Msanii huyo aliandika dogo langu kazini kwa sababu ananipenda na kunikubali lazima tutaimba wote wimbo mmoja kwa ajili yenu na ni kwa vile hata mimi naipenda sauti yake.

Kauli hiyo imekuwa ni ishara tosha kuwa yawezekana kuna mpango wa kufanya kazi kwa pamoja.

Msanii Recho amekuwa akifananishwa sana RayC kutokana na style za uimbaji wao,uchezaji,sauti na hata muonekano wao ingawa Rayc kwa sasa ameonekana kunenepa.


Axact

Post A Comment: