Articles by "michezo_burudani"
Showing posts with label michezo_burudani. Show all posts
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Meneja wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson anaamini Leicester City wanastahili kutawazwa mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Leicester wamekuwa na msimu mzuri 2015-2016 wakiwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano huku wakiwa wamebaki na mechi saba.

Msimu uliopita wote ulikuwa wa wasiwasi kwa Leicester kwani walikuwa wakipigania kutoshuka daraja lakini hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu.

Hata hivyo, kutokana na hali na moyo wa kujituma walio onyesha chini ya Claudio Ranieri msimu huu, Ferguson anadhani hakuna timu inayostahili kushinda taji la ligi zaidi ya Leicester.

Ferguson ambaye alinyakuwa mataji 13 ya ligi akiwa na United amesema kwa uwezo mkubwa walioonyesha Leicester hana shaka kuwa wanastahili kushinda taji hilo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesikitishwa na kikosi chake kukosa ubunifu baada ya kufungwa 2-1 Uholanzi.
Kipigo hicho kimekuja baada ya Uingereza kuonyesha kiwango bora wakitoka nyuma na kuwafunga mabingwa wa dunia Ujerumani mabao 3-2.
Akizungumza baada ya mchezo huo Hodgson amesema pamoja na kumiliki vyema mpira lakini wachezaji wake hawakuwa wabunifu jambo lilichangia kutotengeneza nafasi za kutosha.
Meneja huyo aliongeza kuwa hawakucheza vyema kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Ujerumani kule Berlin.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Uingereza katika Uwanja wa Wembley tangu Novemba mwaka 2013.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania inaendelea leo kwa michezo miwili katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Azam FC watakua kwenye uwanja wao wa Azam Complex kuwakaribisha maafande wa Tanzania Prisons.
Mabingwa wa Tanzania bara Yanga wao watakua wenyeji wa Ndanda FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kila timu ikihitaji ushindi katika michezo hiyo ili kuweza kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.
Aprili 11, Simba SC watakamilisha hatua ya robo fainali kwa kucheza na wagosi wa kaya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwadui FC ndio timu pekee mpaka sasa ambayo imeshafuzu kwa hatua ya nusu fainali, baada ya kuwachapa Geita Gold kwa mabao 3 -0.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) atawakilisha Tanzania mwakani kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Mlinzi wa kilabu ya Manchester City Martin Demichelis ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza kwa madai ya kucheza kamari.
Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 anatuhumiwa kwa kukiuka sheria 12 zinazohusiana na mechi kati ya tarehe 22 na 28 Januari 2016.
Demichelis ana hadi Aprili 5 kujibu shtaka hilo dhidi yake.
Hatahivyo hakuna pendekezo la iwapo shtaka hilo linahusiana na mechi 25 za ligi na kombe la ligi ambazo ameshiriki msimu huu.
Sheria mpya zilizoanza kutekelezwa msimu wa 2014-2015 zinamaanisha kuwa wachezaji na makocha wanazuiliwa kushiriki kucheza dau katika mechi yoyote duniani.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lina uwezo ya kumpiga faini ama hata kumpiga marufuku mtu yeyote atakayekiuka sheria.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Hatua ya mchezaji maarufu wa soka duniani Lionel Messi kutoa viatu vyake viuzwe kusaidia watu wasiojiweza imeibua mjadala mkali nchini Misri.
Messi alifanya hivyo akidhani labda kwamba alikuwa anafanya hisani bila kufahamu kwamba viatu huwa na maana nyingine nchini Misri na pia katika mataifa ya mengine ya Uarabuni.
Wakati wa mahojiano ya runingani ''katika kipindi cha Yes am Famous'' kinachopeperushwa hewani na runinga ya MBC Misri, mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao kwamba angependa kutoa viatu vyake vipigwe mnada.
Kitendo chake kilipokelewa tofauti kabisa na wiki chache zilizopita alipopongezwa na kusifiwa sana kwa kutimiza ndoto ya kijana mmoja wa Afghanistan alipomtumia mpira na fulana yake.

Alipokuwa akivitoa viatu vyake Misri, hakujua kwamba viatu huchukuliwa kama matusi au kukosea watu heshima katika maeneo mengi ya Mashariki ya Kati.
Muda mfupi baadaye wakazi wa maeneo hayo walimkashutumu sana kupitia mitandao ya kijamii.
 Na ili kujibu matusi hayo mbunge mmoja wa Misri said Hassin anayetangaza kipindi kwa jina 'Infirad' alitoa kiatu chake na kusema kwamba atampatia Messi.
Chanzo BBC
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine alikuwa kwenye kiwango cha juu baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kupata ushindi wa magoli 2-01 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ubelgiji uliopigwa Jumanne usiku.
Ndani ya dakika 10 za kwanza, Ronaldo alifanya shambulio la hatari lililomuacha hoi beki wa Ubelgiji Jason Denayer.
Ronaldo alitengeneza nafasi mbili za kupachika bao laikini timu yake ilishindwa kufanya hivyo kutokana na uimara wa golikipa wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Thibaut Courtois.
Hatimaye Ureno ilipata bao dakika ya 20 lililofungwa na Nani kabla ya Cristiano Ronaldo kupachika bao la pili dakika tano kabla ya kwenda mapumziko.
The Real Madrid superstar headed home from a João Mário cross and celebrated in typical style.

Superstar huyo wa Real Madrid alifunga bao lake kwa kichwa akiunganisha krosi ya João Mário kisha kushangilia kwa style ya aina yake. Hilo ni bao la 47 kwa Cristiano Ronaldo msimu huu.
Romelu Lukaku aliifungia Ubelgiji goli la kufutia machozi akiunganisha kwa kichwa krosi ya mdogoake Jordan Lukaku
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Timu ya Taifa ya Vijana Tanzania inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya vijana ya Misri
Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti Boys ya Tanzania dhidi ya The Pharaohs ya Misri utachezwa siku ya Jumamosi, Aprili 2 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa pili utachezwa Jumanne Aprili 5 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Msafara wa The Pharaohs unatarajiwa kuwasili Alhamis tarehe 31, Machi ukiwa na watu 33, wakiwemo wachezaji 25 pamoja na viongozi 8, na wataondoka nchini tarehe 6 Aprili kurudi kwao nchini Misri.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa wakishauriwa na Jan Poulsen, kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume, zilipo ofisi za Makao za Makuu ya TFF.
Serengeti Boys ilingia kambini takribani wiki mbili zilizopita katika hosteli za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki ya kujipima nguvu kujiandaa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.
Tanzania itaanza kuwania kufuzu kwa fainali hizo mwishoni mwa mwezi Juni, kwa kucheza dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana ya Shelisheli.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)








Hatimaye kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin amekamilisha vipimo tayari kujiunga na Manchester United wiki hii.


Schneiderlin ambaye alikua akiwaniwa na klabu za Arsenal, Manchester United na Tottenham Hotspur, amefikia tamati baada ya kutua Carrington uwanja wa mazoezi wa United, kufanyiwa vipimo tayari kwa kuuvaa uzi wa klabu hiyo.

Schneiderlin mwenye miaka 25 alikuwa kiungo wa pili nyuma ya kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic kwa ‘tackling’ nyingi msimu uliopita.

Morgan Schneiderlin, raia wa Ufaransa atakua ametimiza ndoto zake za kucheza klabu bingwa Ulaya, kwani ndicho kilichomuondoa Soton.

Awali Southampton walikataa ofa ya pauni 20m kutoka kwa Manchester United, kwa kuwa wanaamini thamani ya kiungo huyo mkabaji ni zaidi ya paundi milioni 25.

Aidha huo ni usajili wa nne wa klabu hiyo ya Manchester msimu huu mara baada ya kuwanasa tayari, Memphis Depay, Matteu Darmian na Bastian Schweinsteiger.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa bado Manchester United inasaka saini ya mlinzi wa Real Madrid, Sergio Ramos ili wakamilishe usajili wao.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)





Wakala wa Golikipa wa Manchester United, Victor Valdes amesema hajafanya mazungumzo yoyote na klabu ya Uturuki ya  Antalyaspor, lakini amethibitisha kuwa timu hiyo inawinda saini ya Mhispania huyo.

Wakala huyo anayeitwa, Gines Carvajal amesema: “Nimekuwa na mawasiliano na watu mbalimbali kutoka Uturuki wakitaka mazungumzo ya kumsajili Victor, lakini sijaongea na rais wa klabu ya Uturuki”.

Akuzungumza zaidi na AS ameongeza: “Sijui. Sina mpango wa kuzungumza na mtu yeyote kwasababu mchezaji hajavutiwa kwenda Antalyaspor.

“Anatamani kuendelea kubakia Manchester United na amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake”.

“Hatuoni sababu ya kuondoka klabuni hapo. United ni miongoni mwa timu mbili au tatu bora zaidi duniani.

‘Victor anajipanga kupigania nafasi ya kuanza msimu ujao na anahitaji kuisaidia timu kadri atavyoweza”.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)





Klabu ya Manchester City ya Uingereza imekubaliana na wapinzani wao Liverpool dau la pauni milioni £49 kumsajili mshambulizi Raheem Sterling.

Uhamisho wa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa unategemea makubaliano baina yao na vipimo vya afya.

Sterling alikuwa ameomba kundoka Anfield kabla ya klabu hiyo kukataa dau mbili za Man City mwezi Juni.

Mshambulizi huyo atakuwa mchezaji aliyegharimu pesa nyingi zaidi raia wa Uingereza baada yake kukatalia mbali mshahara wa pauni laki moja kwa juma kutoka Liverpool.

Sterling aliyejiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 15 kutoka QPR mwezi februari mwaka wa 2010 yuko katika kandarasi inayokamilika mwaka wa 2017.
QPR inatarajiwa kupokea asilimia 20% ya ada ya kukuza kipaji chake kutoka kwa pesa hizo.

Jumamosi iliyopita ,Sterling alikuwa ametajwa katika kikosi kitakachozuru Thailand, Australia na Malaysia, lakini jina lake likaondolewa.

Wachezaji kadha wakongwe wa klabu hiyo wamemkashifu kwa kutaka kuihama klabu hiyo tangu kocha Brendan Rodgers na mkurugenzi mkuu Ian Ayre kutangaza kuwa alikuwa na nia ya kuihama.

Hivi majuzi utafiti ulimorodhesha kama mchezaji mwenye thamani zaidi barani ulaya.
Mchezaji wa Paris St-Germain Marquinhos alikuwa wapili huku Memphis Depay aliyeihamia Manchester United akiorodheshwa tatu bora.