Uhamisho wa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa unategemea makubaliano baina yao na vipimo vya afya.
Sterling alikuwa ameomba kundoka Anfield kabla ya klabu hiyo kukataa dau mbili za Man City mwezi Juni.
Mshambulizi huyo atakuwa mchezaji aliyegharimu pesa nyingi zaidi raia wa Uingereza baada yake kukatalia mbali mshahara wa pauni laki moja kwa juma kutoka Liverpool.
Sterling aliyejiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 15 kutoka QPR mwezi februari mwaka wa 2010 yuko katika kandarasi inayokamilika mwaka wa 2017.
QPR inatarajiwa kupokea asilimia 20% ya ada ya kukuza kipaji chake kutoka kwa pesa hizo.
Jumamosi iliyopita ,Sterling alikuwa ametajwa katika kikosi kitakachozuru Thailand, Australia na Malaysia, lakini jina lake likaondolewa.
Wachezaji kadha wakongwe wa klabu hiyo wamemkashifu kwa kutaka kuihama klabu hiyo tangu kocha Brendan Rodgers na mkurugenzi mkuu Ian Ayre kutangaza kuwa alikuwa na nia ya kuihama.
Hivi majuzi utafiti ulimorodhesha kama mchezaji mwenye thamani zaidi barani ulaya.
Mchezaji wa Paris St-Germain Marquinhos alikuwa wapili huku Memphis Depay aliyeihamia Manchester United akiorodheshwa tatu bora.
Post A Comment: