2016-03-27
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Meneja wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson anaamini Leicester City wanastahili kutawazwa mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Leicester wamekuwa na msimu mzuri 2015-2016 wakiwa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano huku wakiwa wamebaki na mechi saba.

Msimu uliopita wote ulikuwa wa wasiwasi kwa Leicester kwani walikuwa wakipigania kutoshuka daraja lakini hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu.

Hata hivyo, kutokana na hali na moyo wa kujituma walio onyesha chini ya Claudio Ranieri msimu huu, Ferguson anadhani hakuna timu inayostahili kushinda taji la ligi zaidi ya Leicester.

Ferguson ambaye alinyakuwa mataji 13 ya ligi akiwa na United amesema kwa uwezo mkubwa walioonyesha Leicester hana shaka kuwa wanastahili kushinda taji hilo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Mwanaume mmoja muuza mchanga amepoteza maisha kwa kuchomwa kisu shingoni na kifuani katika kilabu cha pombe za kienyeji mkoani mwanza baada ya kuhisiwa kutembea na mke wa mtu.
Tukio hilo limetokea tarehe thalathini katika kilabu kinachojulikana kama JRC mtaa wa Iloganzala wilaya ya Ilemela mKoani humo ambapo mwanaume huyo ametajwa kuwa ni mkazi wa Butuja mkoa wa Mwanza.
Habari zaidi zinasema mwanaume aliyefanya tukio hilo Pius Paschal alimtuhumu mrehemu kuwa alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mkewe Veronica Jonas (33) hali iliyowatenganisha tangu august 2015 ambaye naye alikuwepo kilabuni hapo.
Baada ya ubishani Pius aliamua kumchoma kisu marehemu huyo na kupoteza maisha papohapo huku mwanaume mwingine aliyejaribu kuamua ugomvi huo Nchama Wanda akichomwa kisu tumboni na utumbo wake kutoka kisha kukimbizwa hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Tayari jeshi la polisi linamshikilia mwanamke anayedaiwa kusababisha ugomvi huo huku likiendelea kumsaka mwanaume aliyetekeleza mauaji hayo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Mwanaume mmoja mkoani Mwanza amepoteza maisha kwa kushambuliwa na wananchi akituhumia kuiba debe mbili za mahindi.
Tukio hilo limetokea tarehe ishirini na tisa katika kijiji cha Ishishangoro kata ya Sima walaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Siku ya tukio mwanaume huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri (40 – 45)  alikutwa na mahindi debe mbili anayosadikiwa kuyaiba kutoka katika nyumba ya Laurent Msangwa mkazi wa eneo hilo.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya wakazi waliamua kumshambulia hadi kuondoa uhai wake.
Tayari jeshi la polisi linaendelea na hatua nyingine za kisheria.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


 
Kamanda wa polisi kanda ya Tarime/Rorya Andrew Satta
Jeshi la polisi katika kanda maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawasaka watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka wasichana wawili katika eneo hilo.
Kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Andrew Satta amesema tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya msingi Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime (jina limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani kutoka shuleni siku hiyo ya machi 26.
Kamanda Satta ameeleza kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu wawili waliokuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata kwa nguvu, kumburuza vichakani na kumbaka kwa zamu wakiwa wamemfunga kitambaa mdomoni.
Baada ya kumaliza tukio hilo walitokomea kwenye vichaka na kutorokea mahali pasipojulikana .
Katika tukio la pili, usiku wa siku hiyo katika kijiji cha Ruhu kwenye mwalo wa wavuvi wilayani rorya, msichana mwenye umri wa miaka 21 (jina limehifadhiwa), alidanganywa na vijana wanne kuwa aliitwa na rafiki yake wa kiume, jambo lililomfanya awaombe wamsindikize alipo na walitii.
Kamanda Satta amesema bila kujua nia ya vijana hao kumdanganya hivyo, binti huyo ambaye hata hivyo anawatambua na kufahamu majina yao, alikubali na kuondoka nao.
Alisema kuwa baada ya kufika kwenye eneo la mwalo wa wavuvi, karibu na vichaka, huku kukiwa na giza nene, waliamua kumbaka kwa zamu na kumwacha akiwa hoi vichakani,
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Paul Kagame, Kanali Tom Byabagamba, amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na kuvuliwa cheo chake baada ya kupatikana na hatia ya kuharibia sifa nchi hiyo na kuhamasisha wananchi kupinga utawala.
Kesi hiyo ilimhusisha pia brigedia jenerali mstaafu Frank Rusagara ambaye naye amepatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 20 jela.
Maafisa hao wa jeshi wamepinga hukumu hiyo wakisema mashtaka dhidi yao yalichochewa kisiasa.
Mahakama imeunga mkono hoja za upande wa mwendesha mashtaka kwamba mlinzi wa muda mrefu wa Rais Kagame, Kanali Byabagamba, alihusika na makosa matatu ambayo ni kueneza kampeni za chuki dhidi ya utawala ambazo zingesababisha wananchi kugoma dhidi ya serikali ya nchi hiyo na kutoheshimu bendera ya nchi hiyo.
Brigedia jenerali mstaafu Frank Rusagara naye amepatikana na makosa kama hayo pamoja na kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Awali alikiri kumiliki bastola mbili alizopewa kama zawadi na nchi za Afrika Kusini na Israel, wakati alipokuwa afisa mkuu anayehusika na ununuzi wa silaha katika wizara ya ulinzi ya Rwanda.
Maafisa hao wamekata rufaa baada ya mahakama kutangaza hukumu hiyo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Marehemu mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.

Na hivyo akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Marehemu Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al shabab.
Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu.

Hapo ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao.
Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi.

Kwa bahati mbata Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja.
Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)




Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Nyasaka B jijini Mwanza wapo hatarini kuathirika kiafya kutokana na kutumia maji ya mto kutpikia na kunywa. 

Wakazi hao wanasema maji yalitoka siku chache mara baada ya kuripoti taarifa yao juu ya uhaba wa maji katika eneo hilo na baadaye kutoweka.

Baadhi ya wakazi katika eneo hilo  wanasema kwa sasa wako njiapanda hali inayowalazimu kunywa maji ya mtoni.

Kwa kuwa tatizo hilo lipo kwa muda mrefu na bado hakujapatikana suluhu ya kudumu, wenyeji wa eneo hili wanatamani kuhama kwa kuwa wanahisi kuwa wameachilizwa na serikali.

Jembe fm inaendelea na jitihada kuwasiliana na uongozi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kujua hatua zilizopo kwa sasa.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


 
Raisi Mafuli alipowasili uwanja wa ndege jijini Mwanza
Wakazi wa vijiji  vya ukanda wa Igombe na Kayenze wilayani Ilemela mkoani Mwanza wamesema kufunguliwa kwa baabara inayounganisha maeneo hayo na Mwanza mjini kupitia uwanja wandege kumesaidia sana kutatua changamoto ikiwemo swala la huduma za afya.
Kabla ya kufunguliwa kwa barabara hiyo wakazi hao walisema walihangaika kufikia huduma za afya kwa kuwa walilazimika kutembea umbali mrefu pia kupanda kwa nauli hli iliyowaweka katika wakati mgumu.
Mbali na hivyo wamesema walikabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo vipigo kutokana na kutumia barabara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongela amesema bada ya kukamilika kwa zoezi la kufungua barabara hiyo hivi sasa wanashughulikia swala la nauli.
Naye meneja wa wakala wa barabara (Tanroad) mkoa wa Mwanza injia Leonard Kadashi amesema tayari wamekwishaanza mpango wa kuikarabati barabara hiyo.
Kushughulikiwa kwa barabara hiyo kunaondoa malalamiko na adha za muda mrefu walizopata wakazi hao.