Mwanaume mmoja mkoani Mwanza
amepoteza maisha kwa kushambuliwa na wananchi akituhumia kuiba debe mbili za
mahindi.
Tukio hilo limetokea tarehe ishirini
na tisa katika kijiji cha Ishishangoro kata ya Sima walaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Siku ya tukio mwanaume huyo ambaye
jina lake halikufahamika mara moja anayekadiriwa kuwa na umri (40 – 45) alikutwa na mahindi debe mbili anayosadikiwa
kuyaiba kutoka katika nyumba ya Laurent Msangwa mkazi wa eneo hilo.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya wakazi
waliamua kumshambulia hadi kuondoa uhai wake.
Tayari jeshi la polisi linaendelea
na hatua nyingine za kisheria.
Post A Comment: