Mwanaume mmoja
muuza mchanga amepoteza maisha kwa kuchomwa kisu shingoni na kifuani katika
kilabu cha pombe za kienyeji mkoani mwanza baada ya kuhisiwa kutembea na mke wa
mtu.
Tukio hilo
limetokea tarehe thalathini katika kilabu kinachojulikana kama JRC mtaa wa Iloganzala wilaya ya Ilemela
mKoani humo ambapo mwanaume huyo ametajwa kuwa ni mkazi wa Butuja mkoa wa Mwanza.
Habari zaidi
zinasema mwanaume aliyefanya tukio hilo Pius
Paschal alimtuhumu mrehemu kuwa alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa
muda mrefu na mkewe Veronica Jonas
(33) hali iliyowatenganisha tangu august 2015 ambaye naye alikuwepo kilabuni
hapo.
Baada ya ubishani Pius
aliamua kumchoma kisu marehemu huyo na kupoteza maisha papohapo huku mwanaume
mwingine aliyejaribu kuamua ugomvi huo Nchama Wanda akichomwa kisu tumboni na
utumbo wake kutoka kisha kukimbizwa hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Tayari jeshi la
polisi linamshikilia mwanamke anayedaiwa kusababisha ugomvi huo huku
likiendelea kumsaka mwanaume aliyetekeleza mauaji hayo.
Post A Comment: