2013-06-09
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
BAADA YA KUDAIWA KUKASHIFU MSIBA WA MAREHEMU NGWEA MSANII OMMY DIMPOZ AFUNGUKA  YA  MOYONI


Msanii Ommy Dimpozi amesema sababu ya kuandikwa vibaya katika vyombo vya habari imetokana na kushindana kibiashara.

Akizungumza kupitia kipindi Cha Extra Vaganza cha Afya radio Mwanza leo hii msanii huyu amesema hali hiyo imesababishwa na yeye kukataa kufanya show iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya vyombo vya habari  (jina tunalihifadhi ) ambapo amedai malipo yalikuwa chini ukilinganisha na matakwa yake.

Kufuatia hali hiyo Ommy Dimpoz ameeleza kampuni hiyo iliamua kumuandika vibaya kwa lengo la kumchafua kama moja ya sehemu ya kumkomoa ili wakati mwingine asipingane nao.

Ameeleza amesikitishwa sana na hali hiyo kwani kilichoandikwa si kweli na kuwa kimetengenezwa ili kumdhoofisha.

Ameongeza yeye kama msanii sanaa ni kazi yake na kuwa anafanya kwa ajili ya maslahi kama ilivyo kwa watu wengine wanapokuwa katika ofisi zao na kuwaomba mashabiki wamuelewe na kutomchukulia vibaya.

Mapema wiki hii kumekuwepo na taarifa zinazodai kuwa Ommy Dimpoz amekuwa na dharau na pia kiburi hata kukashifu wenzie kutokana na kuwa mmoja kati ya wasanii walio kwenye chati ya juu kwa sasa.
Juhudi za kuwatafuta wahusika kuzungumzia swala hili zinaendelea.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

RATIBA YA MAZISHI YA MSANII LANGA

KILEO



Mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa hiphop Tanzania Langa Kileo unatarajiwa kuzikwa mapema juma tatu ya wiki ijayo majira ya saa kumi jioni mara baada ya shughuli za kumuaga zitakazoanza siku hiyo majira ya saa saba mchana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia blogu hii ni kuwa msiba wa marehemu upo nyumbani kwa wazazi wake  maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hosp ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production.

Itakumbukwa sana nyota ya  marehemu Langa ilianza kuonekana na kung'ara kupitia shindano la cocacola pop star ambapo kwa Tanzania alikuwa ni mmoja kati ya washindi watatu ambao waliunda kundi la pamoja lililojulikana kama WAKILISHA.

Katika kundi hilo alikuwa yeye, Witness pamoja na Shaa ambao walifanikiwa kutoa heat kama hoi na Swanglish na baadae kila mmoja kufanya kazi zake kama solo artist.

Msanii Langa Kileo amefariki hapo jana tarehe 13/ 06/2013 kwa ugonjwa wa malaria kali ikiwa ni muda mfupi baada ya mazishi ya msanii mwingine wa muziki huo Albert Mangwea.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

PRODUCER WA “DEAR GOD”  DEEY CLASSIC AMESEMA MENSEN ALISTAHILI TUZO





Producer wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini anyefanyia shughuli zake jijini Mwanza Deey Classic amesema Producer Mensen Selector wa defertality music aliyekuwa mshindani wake alistahili kuchukua tuzo katika kipengele cha producer anayechipukia.

Akizungumza katika kipindi cha hot mix cha EATV hapo jana producer huyu amesema kutokana na kufahamika kwa Mensen sambamba na uwingi wa kazi alizofanya kufahamika na kupata air time kumefanya apate tuzo hiyo kwa urahisi.

Amesema kilichomuangusha yeye ni kutofahamika sana kwa watu kutokana na kutotokea sana katika medias licha ya kusikika kwa jina lake katika baadhi ya nyimbo ambazo amezifanya.

Mbali na hilo mproducer huyu amesema yeye anajiamini na kuwa haoni tabu kufanya kazi katika mkoa wowote tofauti na Dar es salam kama ilivyo kwa maproducer wengi.

Akizungumzia producer anayemkubali alisema anatamani kuwa kama  producer P funk wa bongo recrd kutokana na ubora wa kazi zake.

Deey Classic ametengeneza nyimbo nyingi kama Dera God iliyochukua tuzo tatu pia beat ya wimbo wa msanii young killer aliowashirikisha Stamina na Quick Racka “Jana na leo” na nyingine nyingi.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

TIMBULO : "SINA MAKOSA" SIKUUTUNGA KWA AJILI YA  JACK




Msanii wa bongo fleva Timbulo amesema wimbo wa SINA MAKOSA anaotamba nao hivi sasa hakuutunga kwa ajili ya kumuimbia aliyekuwa mpenzi wake Jack Pentezel.

Timbulo amesema licha ya wimbo huu kuwa na story ya ukweli ndani yake lakini haikuwa kwa ajili ya Jack isipokuwa kuna mpenzi wake mwingine ambaye alidai hata akimtaja hatuwezi kumuelewa kwani si maarufu.

Amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na watu maarufu kwani anajua matatizo yao.

Amesema kwa bahati nzuri nyimbo zake nyingi zina uhalisia na ameimba kwa hisia kwa hivyo hakuna sababu kwa mashabiki wake kufikiria hivyo.

Timbulo amesema haya baada ya swali aliloulizwa na muandishi wa blogu hii lililotokana na kuwepo kwa tetesi kuwa aliutunga kwa ajili ya kumbembeleza mpenzi wake huyo wa zamani.

Msanii huyu amesema hivi karibuni anatarajia kuachia video ya wimbo huo.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

JOSLIN : NAFURAHISHWA SANA  NA USHINDANI ULIOPO   KWENYE GEMU YA MUZIKI BONGO FLEVA





Msanii wa muziki wa kizazi kipya Joslin amesema anafurahishwa na ushindani aliopo kwanye muziki wa bongo fleva kwani unamfanya msanii kufikiria zaidi ni namna gani anaweza kuboresha zaidi kazi yake.

Joslin amesema ushindani huu unaleta changamoto kwa wasanii ukilinganisha na kipindi kile ambacho wasanii walikuwa wachache na hakukuwa na ushindani mkubwa.

Ameeleza hivi sasa gemu imebadilika inalipa tofauti na zamani na inahiaji akili ya ziada  na endapo mtu hatokuwa makini lazima atapotea.

Kuhusu ukimya wake Joslin amesema umetokana na kutingwa na shughuli nyingine pia kujipanga kwani sanaa inahitaji utulivu na huwezi kutoa ngoma kila siku.

Mbali na hilo pia msanii huyu amewaomba mashabiki wake kukaa tayari kumpokea tena kwani yuko mbioni kuachia ngoma mpya.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

NEY WA MITEGO: SIKUWA NA MAWAZO NA TUZO ZA KTMA





Msanii Ney Wa Mitego amesema hakuwa amezichukulia kwa umuhimu tuzo za Kilimanjaro music award licha ya kupata tuzo.

Akizungumza na muandishi wetu msanii huyu amesema tuzo hizo hazikuwa kwenye akili yake na kuwa aliamua kuendelea na shughuli zake za kimuziki mkoani Mbeya kwa mujibu wa ratiba yake.

Ameongeza kwa kuwa wamegundua kuwa ana uwezo mkubwa kimuziki na hata kumpa tuzo ni jambo zuri na la kumshukuru Mungu.

Vilevile msanii huyu akatoa shukurani kwa mashabiki kwa kumpigia kura na kuwaomba waendelee kuwa naye kwani bila wao yeye sio kitu.

Mbali na hilo msanii huyu amesema yeye na Diamond wapo katika harakati za tour ya muziki gani ambayo wanatarajia kuzunguka karibu mikoa yote Tanzania.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

LINAH : NAWAOMBA MASHABIKI WANGU WA MWANZA MSINIELEWE VIBAYA





Msanii Linah kutoka nyumba ya vipaji THT amewaambia  mashabiki wake wa jiji la Mwanza kuwa wasimuelewe vibaya kutokana na kutotokea katika show iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii licha ya kutangazwa kuwa angekuwepo.

Linah amesema hakuwa na taarifa na show hiyo na kuwa alipata taarifa toka kwa baadhi ya watu kuwa yeye ni mmoja kati ya watu waliotajwa kufika kati ya watu waliotajwa kufikayika katika moja ya hoteli kubwa na maarufu jijini humo.

Ameongeza sio yeye tu bali pia wasanii wengine kama Recho,Roma pia hawakuwa wanajua licha ya kutajwa na kusema kuwa yeye kama yeye hawezi kufanya uhuni na endapo kutakuwa na show ambayo amehusishwa moja kwa moja ni lazima atatokea.

"Hata siku moja siwezi kuitwa kwenye show na nisitokee kwa sababu hiyo ni kazi na wao ndo watu wa kwanza ambao wanatusapoti katika kazi yetu,ukifanya kitu chochote cha kuwa dis appoint inakuwa haileti picha nzuri kwa hiyo wajue tu kwamba hao watu waliamua tu kutaka kutuharibia lakini sio kwamba tulishndwa kuja kama tungekuwa tumeelewana"
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

MSANII BEN PAUL AONGELEA SABABU ZINAZOFANYA NGOMA ZAKE KUKUBALIKA KILA SIKU.







Msanii Ben Paul amesema siri kubwa inayofanya muziki wake kukubalika kila siku ni mfumo anaoutumia katika utoaji wa nyimbo katika media. Akifunguka na blogu hii  msanii huyu amesema nyimbo zake huchukua zaidi ya miezi mitano hadi sita baada ya kurekodiwa na kisha kusambaza katika media tofauti tofauti.

Ameeleza hali hiyo humpa muda wa kuamua ni ngoma gani atoe na ipi isubiri au ipi inahitaji marekebisho ili atoe wimbo wenye kueleweka na kukubalika kwa mashabiki.

"Ukiangalia ngoma ya Jikubali nimeiachia hivi karibuni na  hadi sasa tayari kuna ngoma nyingine mpya  nimeishaiandaa itakayofuata baada ya hii ya jikubali"

Msanii huyu ni mmoja kati ya wasanii ambao wameibuka na tuzo za kilimanjaro music Award kwa kazi zilizofanyika 2012/ 2013.


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
WASANII DOGO JANJA NA DOGO D WAFUNGUKA MAGUMU WALIYOKUTANA NAYO






Msanii dogo D kutoka kundi la Wakubwa wa jiji amewashauri wasanii ambao hawajatoka kujiamin na kutokata tamaa kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo.

Kupitia show ya Extra Vaganza ya Afya radio  msanii huyu amesema wasanii wengi wamekuwa wakishindwa kuhimili vishindo vya majaribu na kupoteza ndoto zao kitendo kinachowafanya waendelee kuhangaika mtaani hali ya kuwa wana vipaji.


Akitolea mfano wa aliyokutana nayo Dogo D amesema aliwahi kubaniwa kurekodi kwa kisingizio cha umri na mengine mengi ikiwamo kudharauliwa, hata hivyo hakukata tamaa na kuendelea mbele kitendo kilichoanza kumpa mafanikio leo.


Kwa upande wake Msanii Dogo janja amewaomba mashabiki wa muziki kuthamini wasanii wa nyumbani na kuwasapoti ili kuwatengenezea maisha.


Amesema kwa upande wake yeye nyumbani Arusha anapata sapoti kubwa hivyo angependa kuona na wengine wakipewa sapoti katika mikoa yao kama anayoipata yeye.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

 MSANII RACHEL AWAFUNGUKIA WASANII WADOGO  


 



Msanii Rachel toka nyumba ya vipaji THT amewashauri wasanii wanaoingia kwenye game ya muziki kutowashirikisha wasanii wakubwa na badala yake watoke wao kama wao.

 Akizungmza na muandishi wa blogu hii hivi karibuni msanii huyu amesema kitendo hicho kinawafanya waonekane wamepewa lifti (wanabebwa) na wasanii hao.

Ameeleza ni vyema wakajipanga na kutoka wao kama wao ili kuuonesha uma kuwa wana vipaji na wanaweza bila kubebwa.

" mfano kama mimi namshukuru Mungu kwani nimeweza kutoka na kukubalika bila kumshirikisha msanii mwingine hivyo hata wao wanaweza".

Ameeleza wasanii wengi humfuata wakiomba wamshirikishe kwenye nyimbo zao lakini huwa shauri waimbe wao kama wao ili kujitengenezea taswira nzuri kwa mashabiki.

Pia akamshauri msanii Shilole kuwa safari hii asishirikishe msanii mwingine na atoke yeye kama yeye ili aoneshe ubora wake kwani alipofikia hivi sasa anaweza kufanya yeye kama yeye .