MSANII BEN PAUL AONGELEA SABABU ZINAZOFANYA NGOMA ZAKE KUKUBALIKA KILA SIKU.
Msanii Ben Paul amesema siri kubwa inayofanya muziki wake kukubalika kila siku ni mfumo anaoutumia katika utoaji wa nyimbo katika media. Akifunguka na blogu hii msanii huyu amesema nyimbo zake huchukua zaidi ya miezi mitano hadi sita baada ya kurekodiwa na kisha kusambaza katika media tofauti tofauti.
Ameeleza hali hiyo humpa muda wa kuamua ni ngoma gani atoe na ipi isubiri au ipi inahitaji marekebisho ili atoe wimbo wenye kueleweka na kukubalika kwa mashabiki.
"Ukiangalia ngoma ya Jikubali nimeiachia hivi karibuni na hadi sasa tayari kuna ngoma nyingine mpya nimeishaiandaa itakayofuata baada ya hii ya jikubali"
Msanii huyu ni mmoja kati ya wasanii ambao wameibuka na tuzo za kilimanjaro music Award kwa kazi zilizofanyika 2012/ 2013.
Post A Comment: