LINAH : NAWAOMBA MASHABIKI WANGU WA MWANZA MSINIELEWE VIBAYA





Msanii Linah kutoka nyumba ya vipaji THT amewaambia  mashabiki wake wa jiji la Mwanza kuwa wasimuelewe vibaya kutokana na kutotokea katika show iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii licha ya kutangazwa kuwa angekuwepo.

Linah amesema hakuwa na taarifa na show hiyo na kuwa alipata taarifa toka kwa baadhi ya watu kuwa yeye ni mmoja kati ya watu waliotajwa kufika kati ya watu waliotajwa kufikayika katika moja ya hoteli kubwa na maarufu jijini humo.

Ameongeza sio yeye tu bali pia wasanii wengine kama Recho,Roma pia hawakuwa wanajua licha ya kutajwa na kusema kuwa yeye kama yeye hawezi kufanya uhuni na endapo kutakuwa na show ambayo amehusishwa moja kwa moja ni lazima atatokea.

"Hata siku moja siwezi kuitwa kwenye show na nisitokee kwa sababu hiyo ni kazi na wao ndo watu wa kwanza ambao wanatusapoti katika kazi yetu,ukifanya kitu chochote cha kuwa dis appoint inakuwa haileti picha nzuri kwa hiyo wajue tu kwamba hao watu waliamua tu kutaka kutuharibia lakini sio kwamba tulishndwa kuja kama tungekuwa tumeelewana"
Axact

Post A Comment: