Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
posted by Times fm
Linex Sunday Mjeda, mwimbaji mwenye uwezo mkubwa wa kufanya
nyimbo zenye ujumbe mzito wa mapenzi, anatuhumiwa kumshambulia kwa
maneno makali aka matusi member wa Chamber Squad,Mez B wa Area C,
Dodoma.Rafiki wa karibu wa Mez B ambaye ni mtu wa media anayefahamika kwa jina la ‘Maujanja’ aliyekuwa naye muda huo (Jana usiku), ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa mwimbaji huyo wa Kimugina alimtukana Mez B ambaye alishindwa kuvumilia akajikuta alia machozi kama mtoto mdogo.
“Aisee mimi nilikuwa pale mwanangu,maana nilikuwa mimi,Fadhili na demu wangu yaani mke wangu mimi tulikuwa pale tumeenda kula pale Kona Bar.Kwa hiyo tumefika pale…Sasa kuna mtu alikuwa amemshika demu wangu sehemu za mgogoni yaani nyuma.Sasa wife akawa amepaniki pale akaanza kujibishana na yule jamaa ambaye ni dereva tax pale Kona Bar.
“Sasa Fadhili hicho kitendo akawa hajakipenda,sasa katika kujibishana na hao jamaa,Linex alikuwa amekaa meza ambayo tunatazama sasa akawa anatuambia kuwa sasa ninyi ongeeni tu hao jamaa lakini mimi ntapiga mtu bomba hapa..yaani ni kama ninyi mnaongea nao kwa nini msifanye action?”Maujanja amesimulia.
“Sasa Mez B akamaind ile kauli,nafikiri alifikiri jamaa kama alituambia sisi.Kwa hiyo Mez B akawa amefika akamwambia sasa wewe kama umesema utatupiga bomba basi nipige bomba mimi niko hapa..kwa hiyo varangati pale likatokea.” Ameogeza.
Amesema Linex alianza kumtolea maneno machafu Mez aliyejitokeza kumhoji Linex kuhusu kauli zake,lakini mwisho wa siku alijikuta akimwaga machozi kwa kile alichokuwa akikisikia.
“Linex alitukana sana pale, yaani Kona Bar pale palichafuka yaani ilikuwa noma.Linex alikuwa anamtukana Mez B, yeye alikuwa hajibu lakini kwa kweli alilia machozi kabisa...akawa anasema kama ‘Linex yaani unanitukana hivi’.. na vitu kama hivyo.”
Amesema ugomvi uliisha na kila mmoja aliondoka akiwa salama,lakini Mez B amesema kuwa anampango wa kumtafuta Linex mchana kwa lengo la kumhoji kama kweli alimtukana akiwa mzima ama alikuwa amelewa.
Times Fm imemtafuta Mez B lakini namba yake ilikuwa haipatikani kwa muda mrefu, lakini ilifanikiwa kumpat Linex, ambaye alikanusha kuhuma hizo na kudai kuwa hakumbuki.
“Mimi sijafanya kitu kama hicho na sikumbuki. Kuhusiana na Mez B ndiye ananikosea adabu mimi. Na asilete mpango wa kutafuta kick mjini, afanye kazi yake vizuri.”Alisema Mez B kwa ufupi.