Msanii Sajna

Msanii wa muziki kutoka jijini Mwanza Sajna amesema Producer  Kid Bwoykutoka Tetemesha Records anafaa kuwa mfano wa kuigwa.
Akiongea na bongo20 amesema licha ya kuwa kwa sasa hayuko katika managment yake na akifanya kama solo artist msanii huyu ameeleza bado ana uhusiano mzuri na producer huyo na kuwa amekuwa ni mmoja kati ya watu wanaotoa sapoti kubwa katika kusambaza wimbo wake mpya wa "Nisamehe"

"Licha ya kuwa nimeondoka katika management yake lakini bado amekuwa karibu na mimi na kusaidia kusambaza kazi yangu ikiwa ni pamoja na kuweka kwenye blog ya bongo5 kitu ambacho ni tofauti na producers wengine" Alisema msanii Sajna

                      Producer Kid Bwoy

Katika hatua nyingine msanii huyu amewaomba mashabiki wa muziki hapa nchini kupokea kazi yake hiyo mpya na kukaa tayari kupokea kazi nzuri zaidi kutoka kwake.
Axact

Post A Comment: