Taarifa kutoka katika vyanzo vya habari vinasema msanii Justine Bieber alikuwa akihofia siri zake kuvuja baada ya askari waliofika nyumbani kwake
siku ya jumanne wiki hii kwa jili ya kutafuta ushahidi wa tukio la kutupa mayai wakati walipochukua simu yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa Tmz askari hao walichukua simu yake kwa lengo la kutazama kama kuna ujumbe wowote alioutuma kwa watu wake ukizungumzia juu ya tukio hilo ili kupata ushahidi.

Wakati maafande hao wakiwa na lengo la kutazama upande wa ujmbe  imedaiwa msanii huyu alikuwa na wasiwasi mkubwa akihofia picha zake za utupu kusambaa pamoja na taarifa zinazohusianana  madawa ya kulevya.
Hata hivyo ripoti zinasema haikuwa hivyo.
Axact

Post A Comment: