2014-03-02
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Baada ya habari kuenea juu ya kusimamishwa kwa msanii Lord Eyes na kampuni ya Weusi msanii Joh makin aibuka na kupinga taarifa hizo.
Kupitia ukurasa wake wa face book msanii huyo aliandika maelezo mafupi yanayoashiria kupinga taarifa hzo za kufukuzwa ikiwa ni pamoja na picha inayowaonesha wakiwa pamoja.

Joh Makini
“Lordize hajafukuzwa wala kutengwa kama wengi mnavyoitafsiri”.aliandika Joh.
Hata hivo kauli hii inaonesha kuwa tata kutokana na mssanii huyo kutoeleza zaidi ni kitu gani alimaanisha
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Victoria Kimani, mrembo na mwanamuziki raia wa Kenya amekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na CEO wa Wasafi Classic, Diamond Platinumz kufuatia tetesi zilizozagaa baada ya wawili hao kuonekana kwenye picha kadhaa za pamoja.

“Sifahamu hizi tetesi zimetokea wapi. Nilikutana na Diamond mara moja, na ilikuwa wakati tunarekodi wimbo wa ONE Campaign Afrika Kusini wiki mbili zilizopita.” Victoria Kimani aliiambia Nairobi News.

Aliongeza kuwa hata hawajawahi kuwasiliana kwa simu tangu walipomaliza kupiga picha hizo na zaidi hata namba ya Diamond hana.

“Hata sina namba yake, kwa hiyo sijawasiliana nae tangu tulivyokutana Afrika Kusini.”

Hivi karibuni kaka yake Victoria Kimani, Bamboo alitoa maoni/mtazamo yake na kudai kuwa Diamond sio ‘type’ ya Victoria Kimani.

Hata hivyo, Diamond alikuwa wa kwanza kuzikanusha tetesi hizo na kudai kuwa mrembo huyo ni mshikaji wake tu.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Msanii Khalifa Ilunga maarufu kama Cp ameamua kuanzisha record label aliyoipa jina la ‘Brain Storm Music’  itakayosimamia kazi zake pamoja na za wasanii wengine.
Katika mahojiano na Times fm msanii huyo amesema amefikia uamuzi huo ikiwa ni katika kuboresha mwenendo mzima wa kazi zake na za wasanii wengine.
“Nafungua label yangu..music label yangu kwa hiyo niko sasa hivi na-register wasanii na vitu kama hivyo.” alifunguka Cp
“Nimeanzisha label yangu ambayo mimi niko chini yake pamoja na wasanii wengi tu ambao wamekuwa wakinifuata, wakiomba ushauri wakiomba miongozo na misaada ya kifedha. Kwa hiyo wote tutakuwa chini ya uongozi mmoja na shughuli zetu za kisanaa zitakuwa zinashughulikiwa na hiyo label.”
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Baada ya kiongozi wa G-Unit, 50 Cent kumdhihaki hasimu wake wa muda mrefu, Rick Ross kwa kupost picha zinazoonesha kuwa huenda ni shoga, wengi walijua tayari moto umewashwa na kilichobaki kusubiri nini atakachofanya Rick Ross.

Lakini kwa mujibu wa chanzo cha mtandao wa TMZ, rapper huyo ambaye jina lake halisi ni William Leonard Robert II, hataupoteza muda wake kumjibu rapper huyo na kueleza sababu kuwa anamuona 50 Cent hana umuhimu kwake.

Imeelezwa kuwa Rick Ross amepanga kuiacha hiyo issue ipite kimya kimya na yeye aendelee kujikita katika masuala muhimu ya kutengeneza ngoma kali.

Jumapili iliyopita, 50 Cent alipost kwenye Instagram picha inayomuonesha Rick Ross akimsogelea P.Diddy kama vile wanataka ku-kiss na akaandika kwa ufupi, “something ain’t right’.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania anayetokea katika kundi la kampuni ya weusi aitwaye Lord eyes amesimamishwa na kampuni hiyo kwa tuhuma za wizi.
Msemaji wa kampuni hiyo Nick wa pili amesema wameamua kumsimamisha kwa kuwa amevunja utaratibu wa kampuni hiyo.
“Uamuzi wa kumsimamisha tumeufikia jana na leo ndio tumeamua kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana na misingi na makubaliano ya kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na mawazo yetu kwa pamoja ndio yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba tumemsimamisha kutokana na makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni ambayo mengine yatabakia ndani ya kampuni.”alisema Nick wa pili
Msanii Lord Eyes alidaiwa kushikliwa na polisi juma mosi iliyopita kwa tuhuma za wizi wa laptop aina ya Dell.
Habari zaidi zinasema kufuatia tukio hilo msanii wa kike Ray c ambaye ni mpenzi wa zamani wa Lord Eyes ameonesha kuchukizwa na tukio hilo alilolifanya msanii huyo.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Ney wa Mitego
Msanii wa mziki nchini Tanzania Ney Wa Mitego ameamua kulelezea hisia zake juu ya tukio la kiongozi wa mtanashati entertainmet Ostaz Juma kuweka picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa face book ziamuonesha akipigiwa magoti na msanii Pnc.
Katika mahojiano na timse fm Ney wa Mitego alisema kufuatia tukio hilo atamdharau Ostaz kuliko mtu yeyote hapa duniani.
Aliendelea kufunguka zaidi kwa kueleza kitendo hicho kimemgusa zaidi kuliko hata Pnc mwenyewe.
Mimi tangu nilipoona hizo picha nilisema siwezi kumpenda hata siku moja, hata salamu yangu siwezi kumpa. Siwezi kumheshimu hata kidogo. Nitamdharau kuliko kitu chochote, kuliko mtu yeyote aliyewahi kunikosea sana. Ila katika watu ambao waliowahi kunikosea, nafikiri mimi Ostaz Juma amenikosea kupita maelezo. Kuliko alivyomkosea PNC mwenyewe.” Alifunguka Ney
 Msanii huyu anauungana na baadhi ya wasanii pamoja na wadau wa muziki ambao walionekana kukerwa na kitendo hicho wakidai ni udhalilishaji kwa wasanii.