Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania anayetokea
katika kundi la kampuni ya weusi aitwaye Lord eyes amesimamishwa na kampuni
hiyo kwa tuhuma za wizi.
Msemaji wa kampuni hiyo Nick wa pili amesema wameamua
kumsimamisha kwa kuwa amevunja utaratibu wa kampuni hiyo.
“Uamuzi wa kumsimamisha tumeufikia jana na leo ndio tumeamua
kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana
na misingi na makubaliano ya kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na
mawazo yetu kwa pamoja ndio yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba
tumemsimamisha kutokana na makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni
ambayo mengine yatabakia ndani ya kampuni.”alisema Nick wa pili
Msanii Lord Eyes alidaiwa kushikliwa na polisi juma mosi
iliyopita kwa tuhuma za wizi wa laptop aina ya Dell.
Habari zaidi zinasema kufuatia tukio hilo msanii wa kike Ray
c ambaye ni mpenzi wa zamani wa Lord Eyes ameonesha kuchukizwa na tukio hilo
alilolifanya msanii huyo.
Post A Comment: