Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Msanii kutoka nchini Uganda Jose Chameleon amepata dili la kutangaza utalii wa nchi yake. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa face book msanii huyu ameandika maelezo yanayoashiria kuwa amepata dili hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka picha inayomuonesha akiwa pamoja na spika wa bunge la nchi hiyo bi Kadaga Rebeca.Mbali na kupata shavu hilo pia ameteulia kuwa balozi wa shindano la kupanda mwamba wa Kagulu uliopo mkoani Buyele ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyika mapema May 9-10 mwaka huu.