2014-05-18
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul ama Diamond ameendelea kuongoza katika kura za shindalo la tuzo za Black Entertainment Tv ama Bet. kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo hizo Diamond anaongoza kwa zaidi ya asilikia sabini na kuwaacha wenzake kwa mbali. Endapo kura zitaendelea kuwa hivyo msanii huyo ataibuka na tuzo katika kipengele cha International African Act. Tamasha la kutoa tuzo hizo litafanyika July 29 Los Angeles Marekani.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii Nikck mbishi kutoka Tanzania aliyeachia hivi karibuni wimbo mpya alioupa jina la Natoka Tanzania amezidi kupata moyo zaidi baada ya watu maarufu na wanasiasa kuonesha kumuunga mkono katika wimbo huo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika, Shukurani Zito Kabwe kwa kuni follow Aluta continua.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz ameonewhwa kufurahishwa na namna show yao na Diamond ilivyofanyika jijini London. Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo aliandika kuwa asante london show ilikuwa tamu zaidi ya utamu huku akiwa ameambatanisha na kipande cha video kinachowaonesha wakiimba wimbo wa Utamu wa msanii Dully Sykes ambao pia walishiriki. Wasanii hao wamefanya show jijini london usiku wa jumamosi hii ikiwa ni baada ya show yao iliyofanyika jijini Dar es salam siku ya Ijumaa kuamkia juma mosi hii.s