2013-06-23
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

BAADA YA MUZIKI GANI,NEY AJIKUTA NJIA PANDA




Msanii Ney wa Mitego njia panda baada ya kushindwa kuchagua ni wimbo gani ufuate baada ya Muziki gani.

Msanii huyu amesema hadi sasa kuna nyimbo mbili ambazo ni SALAMU ZAO na KWA MASELA na ziko tayari ikiwemo aliyofanya na Diamond na hivyo anahisi kutegemea ushauri toka kwa wadau.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

KALA KUJA NA VINA VYA "MBA"


Msanii Kala Jeremiah aliyetamba na wimbo wa Dear God amesema hivi sasa yupo mbioni kutengeneeza wimbo wenye vina vinavyoishia na neno "mba"

Kupitia ukurasa wake wa Face book msanii huyu amesema katika wimbo huo anatarajia kupata mashairi kutoka kwa mashabiki ambao wanaendelea kumtumia mashairi hayo.

Kila la kheri Kala na tunasubiri tuone tena itakavyokuwa.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

BELEE9 ATOA SOMO KWA MAPRODYUZA




Msanii Belle 9 amewaomba maproducer kukaza uzi zaidi katika kazi wanazozifany ili kuboresha zaidi na kwenda kimataifa.

Akizungumza katika interview na Kiss fm Belle amesema muziki unaofanyika sasa ni mzuri lakini kunahitajika nguvu ya ziada kwa kutengeneza nyimbo zenye ubora wa kimataifa ili kupanua muziki wa Tanzania.

Amefunguka zaidi kuwa kwa upande wa video haoni shida sana kwani kuna baadhi ya nyimbo zinapata air tym katika channel mbali mbali na kubwa nje ya nchi.

Amesema ni muda mzurikwa wasanii na producers kuumiza kichwa ili kwenda zaidi ya Bongo.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

LADY JAY DEE NA Q CHILAH KUJA NA NGOMA 


Huenda ukawa ni ujio mzuri kwa upande wa Q chillah ambaye aliwahi kutamba kipindi cha nyuma na kisha kuonekana kuyumba katika siku za hivi karibuni.
Msanii Lady Jay dee ametweet kuwa yupo jikoni kwa ajili ya pishi la wimbo ambao anaufanya yeye na msanii Q chilla.
Katika tweet hiyo ameambatanisha na picha iliyowaonesha wawili ho wakiwa studio pamoja na Man water.

Hivi ndivyo alivyo tweet tazama  hapo chini

Mtu 3 ndani ya studio. Mwaikumbuka Zamani - Q Chief feat Jide?? Nikilala naotaa, naota km unaniita. Sasa yaja mpya

Lady jaydee,Q chillah na Man water


Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

KAJALA AKANUSHA KUGOMBANA NA


WEMA SEPETU

Wema na Kajala
 
Siku chache baada ya baadhi ya magazeti na bolgs kuripoti kuwa hivi sasa hakuna mahusiano mazuri kati ya wasanii Kajala na Wema Sepetu mmoja wa wasanii hao amekenusha habari hizo.
Msanii huyo anayejulikana kwa jina la Kajala amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Msanii huyu amedai kuwa hakuna ugomvi wowote kati yao na kuwa hamna sababu ya kugombana nae kwani amekuwa msaada kwake na hivyo hajui habari hizo zimetoka wapi.
“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala
Juhudi za kumtafuta Wema kuzungumzia swala hili bado zinaendelea.
Hivi karibuni kuliripotiwa kuwa wawili hawa hawaelewani kutokana na Wema kumbania Kajala kupiga dili mbali mbali ikiwemo ile ya kwenda nchini China.
Itakumbukwa hivi karibuni Wema alitoa kiasi cha shilingi million kumi na tatu kwa ajili ya kumnusuru Kajala kufungwa gerezani.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

MSANII JB KUINUA WASANII WADOGO


Msanii kutoka Bongo movie Jacob Steven au JB amesema ana mpango wa kuwainua wasanii wanaochipukia.

Akizungumza mapema wiki hii msanii huyu amesema yeye na kampuni ya Jerusalem wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuna watu wana vipaji na wanahitaji kusaidia hivyo yeye ameona kuna haja ya kufanya hivyo.

“sisi Jerusalem company tunajua Mungu alipotuweka alituweka ili tushike watu wengine mikono na mpaka sasa hivi nime sign kwenye contract yangu filamu za aina mbili. Kuna filamu ambazo mimi nitashiriki na kuna zingine sitoshiriki kabisa nita direct na ku produce nita tupa ela kuzifanya hizo film kwa ajili ya hawa under grounds” alisema JB.

Jb aliongeza zaidi kuwa kuanzia mwakani atakuwa akitoa filamu tatu ambazo atazicheza yeye mwenyewe na nyingine kumi atakazotoa zitachezwa na wasanii wengine wadogo huku yeye akizisimamia.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni Jb amekuwa ni mmoja wa wasanii wa filamu wa kubwa hapa nchini na wanaokubalika kutokana na uchezaji wao wa filamu na ni mmoja kati ya wasanii waliopata tuzo mwaka huu kupitia movi inayojulikana kwa jina la Nakwenda kwa Mwanangu aliyocheza na msanii wa vichekesho King Majuto huku mzee huyo kuchukua tuzo ya mchekeshaji bora kwa kupitia movi hiyo.
Tuzo nyingine aliyoipata ni muigizaji bora wa kiume katika tuzo zilizoandaliwa na kampuni ya steps.