KAJALA AKANUSHA KUGOMBANA NA
WEMA SEPETU
Wema na Kajala
Siku
chache baada ya baadhi ya magazeti na bolgs kuripoti kuwa hivi sasa hakuna
mahusiano mazuri kati ya wasanii Kajala na Wema Sepetu mmoja wa wasanii hao
amekenusha habari hizo.
Msanii
huyo anayejulikana kwa jina la Kajala amesema taarifa hizo hazina ukweli
wowote.
Msanii
huyu amedai kuwa hakuna ugomvi wowote kati yao na kuwa hamna sababu ya
kugombana nae kwani amekuwa msaada kwake na hivyo hajui habari hizo zimetoka
wapi.
“Unajua
mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na
Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa
sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla
ya kuandika” Alisema kajala
Juhudi
za kumtafuta Wema kuzungumzia swala hili bado zinaendelea.
Hivi
karibuni kuliripotiwa kuwa wawili hawa hawaelewani kutokana na Wema kumbania
Kajala kupiga dili mbali mbali ikiwemo ile ya kwenda nchini China.
Itakumbukwa
hivi karibuni Wema alitoa kiasi cha shilingi million kumi na tatu kwa ajili ya
kumnusuru Kajala kufungwa gerezani.
Post A Comment: