2014-02-09
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Mkali wa RnB mwenye mashabiki wengi wanaopenda aina hiyo ya muziki hususani hapa Tanzania, ameweka wazi jinsi ambavyo analipwa zaidi kwa shows za nyumbani Tanzania kuliko shows za nje ambazo amepata mialiko.
Mkali huyo wa ‘Manenomaneno’ amefunguka katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm wakati akitambulisha rasmi wimbo wake ‘Umenichora’ aliofanya na Fundi Samweli na Joh Makini, na kuutoa mfano hai wa show yake atakayofanya Ujerumani, April  mwaka huu.
“Definitely, nyumbani kuna nguvu sana, mfano mimi mwezi wa nne nina show moja German, lakini hiyo show…inalipa vizuri, lakini trust me navyopata hapa kwenye show ya Bongo ni twice.” Amesema Ben Pol.
Ameeleza hiyo kuwa sababu ya kubadilika na kufanya RnB yenye vionjo vya kitanzania, na kuwashauri wasanii wengine kufanya muziki wa nyumbani ili waweze kupata shows zaidi nje zitakazowalipa pesa nyingi zaidi.
 “Kwa sababu...unajua shows nyingi tunaenda kufanya kama nje, kama unapiga muziki wenye flavour ya nje, ni shida sana kufanya ile classic RnB halafu ukafanya kuliko R Kelly. Kwa mantiki hiyo, tufanye muziki wa nyumbani ili watu wa nje wakisikiliza waseme mbona hatuwezi kufanya muziki kama wa yule. Kwa hiyo kama wakiona kama haiwezi wanaweza kui-add kwenye stream yao kwa kuwa wao wanaona hawaiwezi.”
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Rapper wa Young Money, Drake nae ameelezea uhusiano wake na mwimbaji wa Caribbean Rihanna aka RiRi ambaye aliwahi kuzungumziwa kuwa sababu ya ugomvi mkubwa kati ya rapper huyo na Chris Brown aliyekuwa mpenzi wake.
Drake ambaye jina lake halisi ni Aubrey Drake Graham, alieleza katika interview aliyofanya na jarida la Rolling Stone kuwa yeye na mwimbaji huyo ni marafiki tu wanaufurahia maisha pamoja.
“She’s the ultimate fantasy. I mean, I think about it. Like ‘Man, that would be good’. We have fun together, she’s cool and s**t. But we’re just friends, she’s my dog for life.” Alisema Drake.
Aliongelea pia kuhusu uhusiano wa mapenzi na mpango wa kuwa na mpenzi, ambapo alidai kuwa hana mpango wa kuwa na mpenzi kwa sasa, na kwamba hana mzuka wa kutafuta mapenzi kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita. Na kwamba bado hajakutana na mtu ambaye anayefanya awaone watu wengine hawana mpango.
“I’m not after p***y like I was three years ago, when I was trying to make up for all the years when no girl would talk to me. But I haven’t met somebody that makes everybody else not matter.”
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Msanii kutoka nchini Marekani Nick Minaj ameweka wazi jina la Albamu yake mpya ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mtandao wa Baller status wa nchin humo jina la Albam hiyo ni Pink print.
Hatua hii ya Minaj inakuja ikiwa ni katika muendelezo wa project yake ya Pink themed project.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Hadi hvi sasa bado watu wengi wanashauku ya kutaka kufahamu ni nani hasa baba wa kichanga cha Kim Kardash kiasi cha kujiuliza ni nani hasa baba wa mtoto huyo.
Mapema juma tano wiki hii kuna taarifa zilitoka kupitia mitandao mbalimbali ya habari nchini marekani kuwa msanii Lil kim ni mjamzito.
Taarifa hizi zilidai kuwa msanii huyu ameonekana katika tamasha la New fashion week akiwa ni mjamzito ambapo baadhi ya watu walidai kuwa ameamua kutumia tamasha hilo kuonesha wazi kuwa yeye ni mjamzito.
Hata hivyo pamoja na kuonekana na ujauzito bado hajafahamika mzazi wa kiume wa kichanga cha mwana dada huyo kilichopo tumboni.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Rapper mzawa wa Toronto, Canada, Drake amemchana Ben Haggerty aka Macklemore kwa uamuzi wake wa kuonesha hadharani ujumbe alioumtumia Kendrick Lamar kwa simu baada ya kumshinda kwenye kipengele cha Album Bora ya Rap kwenye tuzo za Grammy mwezi uliopita.
Drake ambaye pia alikuwa akiwania tuzo katika kipengele hicho na album yake ‘Nothing Was The Same’, amefunguka ya moyoni alipokuwa akifanya mahojiano na jarida la Rolling Stone na aliponda kitendo hicho na kumwambia Macklemore kuwa kama alihisi hakustahili basi ajitahidi afanye muziki bora zaidi.
“I was like, ‘You won. Why you posting your text message? Just Chill. Take your W, and if you feel you didn’t deserve it, go get better – make better music.” Alisema Drake.
Mkali huyo wa ‘Started From the Bottom’ alihoji kuwa Macklemore anadhani Kendrick Lamar na wengine waliokuwa kwenye kipengele hicho wangeshinda tuzo hiyo wangemtumia yeye ujumbe?
Hata hivyo, Drake hakuponda kitendo cha Macklemore pekee, aliziponda kiaina tuzo za Grammy na kudai kuwa siku zote katika tuzo hizo huwa hawashindi wasanii bora zaidi katika kiwanda cha muziki.
 Lakini alikiri kuwa hata kama Macklemore na Ryan Lewis walishinda tuzo hiyo kwa njia ipi, ukweli ni kwamba waliwavuta watu wengi zaidi yake yeye, Jay Z, Kanye West na Kendrick Lamar.
Katika tuzo za Grammy 2014, Macklemore & Ryan Lewis walishinda tuzo ya album bora ya Rap ya mwaka ‘Best Rap Album’ na album yao ya ‘The Heist’ na kuzishinda ‘Nothing was The Same’ ya Drake, ‘Yeezus’ ya Kanye West, ‘Magna Carta Holy Grail’ ya Jay Z na ‘Good Kid, m.AA.D City’ ya Kendrick Lamar.
Baada ya kushinda tuzo hiyo, Macklemore alimtumia Kendrick Lamar ujumbe mfupi uliosomeka, “You got robbed. I wanted you to win. You should have. It’s weird and sucks that I robbed you. I was gnna say that during the speech. Then the music started playing during my speech, and I froze.”
Baadae aliupiga picha ujumbe huo na kuuweka kwenye Instagram kuwaonesha watu wote na kuandika, “My text to Kendrick after the show. He deserved best rap album.”
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii nguli wa Bongo fleva Proffesa Jay pamoja na msanii wa nyimbo zenye vionjo vya kiasili Mrisho Mpoto huenda wakatengeneza ladha mpya ya muziki kutokana na kukutana katika kazi moja.
Kupitia ukurawa wake wa mtandao wa kijamii wa face book msanii Proffesor Jay ameandika maelezo yanayoashiria wawili hao kuna kazi wanayoifanya kwa pamoja.
Msanii huyu mbali na maelezo hayo pia ame post picha inayomuonesha akiwa na Mpoto wakiwa katika studio ya Waite records inayomilikiwa na Mrisho Mpoto.

Nimemtembelea mjomba @mrisho mpoto kwenye studio yake ya WAITE RECORD. .. Mambo makubwa sana yanafuata. .STAY TUNED!!


Hatua hii ya ya wasanii hawa imeonesha kuungwa mkono na baadhi ya mashabiki ambao wameamua kuwapongeza.Hata hivyo bado wasanii hawa hawajaweka wazi ni kazi gani wanatarajia kuzifanya kwa pamoja.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii Tunda Man ni mmoja kati ya wasanii ambao wamewahi kukumbwa na hatari ya kuaibika.
Akizungumza na Bongo20 msanii huyu amesimulia namna alivyonusurika kudhalilishwa baada ya kukosa pesa ya kulipia vinywaji pamoja na chakula alichotumia.
Msanii huyu alisema kuna siku alikwenda Kijitonyama katika kiwanja kimoja kwa ajili ya kula na kupata vinywaji,alipofika huko alikutana na baadhi ya jamaa zake ambapo waliungana na kuendelea kukamua.
Kwa muda wote wakiendelea kujiachia wale jamaa zake walikuwa wakitegemea pochi ya Tunda,kuna muda ulifika msanii huyu akaamua kuangalia alio lake kwa waleti ambapo hakukuta kitu na ndipo alipoanza kujiuliza ni nani wa kumsitiri na aibu ambayo inataka kumkumba.
Kwa bahati akapata wazo la kumtafuta Suma Lee ambaye kwa bahati alitokea na kumlipia.
Tunda man alieleza kuwa yote hayo yalimtokea akiwa tayari amekwisha kuwa msanii.
no image
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)


Clifford Joseph Harris Jr. aka T.I, rapper wa Atlanta Marekani, ameshindwa kuvumilia baada ya kuona mke wake ‘Tiny’ amevuka mipaka kwa kupost kwenye Instagram mfululizo wa picha zinazoonesha makalio yake.
Ingawa rapper huyo toka Atlanta alikuwa na uwezo wa kumpigia simu ama kumtumia message mkewe huyo kumuonesha alichokuwa hapendi kwenye picha hizo, jamaa aliona dawa inatakiwa iwekwe pale pale kwenye kidonda! Hivyo akaandika pale pale palipomuudhi!!
“You have so much more going for u other than your a$$. Although it is so magnificent, I think u should spend just as much time showcasing those other things as u do ya #booty…awesome pic thou. Lov.” Ameandika T.I kwenye post hiyo.
Mkewe Tiny nae akamjibu kwa kung’ata na kupuliza, kwa kuwa inasemekana kuwa ameshachoshwa na ugomvi uliopo katika ndoa yake.
Alimjibu kwa kejeli T.I kuwa yeye hakuwa na nia ya kuonesha makalio yake bali alikuwa anataka kuonesha kiuno chake, na kwamba kumbe mmewe alikuwa anaangalia makalio tu.
“I wasn’t showing off my ass in this pic it was about my waist… u just looking at the ass bae! U know I wasn’t saying getting my sh*t together about my ass now don’t U? But glad u like it bae.”
Majibishano hayo kati ya wanandoa na mastaa wa kipindi cha TV cha Family Hustle kinachowaunganisha wao na watoto wao saba, yalisababisha mashabiki wao kushangaa na wengine walitoa ushauri kuwa T.I angetakiwa kutumia simu.
Tangu mwezi uliopita kumekuwa na ripoti kuwa wawili hao wako katika mgogoro mkubwa kiasi cha kusemekana kuwa wanataka kupeana talaka.
Tetesi hizo zilichochewa na picha za Tiny alizopost zikionesha mkono wake wa kushoto ukiwa bila pete ya ndoa. Iliripotiwa pia kuwa mwanamke huyo anaewaelewa watoto saba wa T.I na wake kwa ujumla wao, amekuwa akiparty sana akiwa na rafiki zake, tofauti na zamani.
Kwa undani wa mkasa huu, usikose kusikiliza kipindi cha The Switch cha 100.5 Times Fm Jumamosi hii kuanzia saa sita kamili mchana na Raheem Da Prince.

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii kutoka nchini Tanzania Young d Amesema baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na mtu anayetumia jina lake face book kutapeli watu msanii huyu amedai kupata suluhisho la tapeli huyo.
Msanii huyu ameeleza kuwa ni kwa muda mrefu amekuwa akitafuta namna ya kumtia hatiani mtu huyo bila mafanikio kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha.
Ameeleza hivi sasa tayari amekwishapata mtu ambaye ametapeliwa na mtu huyo kama alivyoshauriwa na askari na kuwa huyo ndiye atakayetia nguvu katika kesi hiyo.
Amefunguka zaidi kuwa pamoja na kumpata mtu huyo aliyetapeliwa tayari ana mwanasheria ambaye atasaidiana naye katika kumfungulia kesi mtu huyo.
Msanii huyu amekwisha fanya jitihada za kumpata mtu huyo anayemuita tapeli kwa kuripoti polisi ikiwa ni pamoja na kutangaza kwa watu kuwa yeyote anayemfahamu mtu huyo ampe taarifa,hata hivyo juhudi zake hazikuonesha mafanikio yoyote.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Siku chache baada ya kuibuka kwa habari kuwa Msanii Linex na Agnes Masogange ambaye ni video queen wa videos hapa bongo,msanii huyu ameamua kutoa uchovu na kuzungumzia swala hili.
Katika maelezo yake aliyoyatoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa face book msanii huyu ameonesha kusikitishwa na habari hizo zinazodaiwa kutlewa na tovuti moja hapa nchini jina kapuni.

“ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Ameandika kwenye Facebook.
Linex anaungana na wasanii wengine wa muziki hapa nchini akiwemo Mirror ambao wamekwisha kumbwa na hali hiyo.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Kumekuwa na tetesi zinazosema kuwa msanii Wema Sepetu ana uhusiano wa kimapenzi na msanii aliye chini ya kampuni yake ya Endless fame msanii Mirror.
Kufuatia uvumi huo msanii Mirror ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia tetesi hizo ambapo amekanusha na kudai kuwa hazina ukweli.
Ameeleza yeye na Wema ni kama ndugu na hakuna chochote kinachoendelea zaidi ya uhusiano wa kazi.
Ameongeza kuwa Wema amekuwa ni mtu mzuri kwake kwa kuwa amemsaidia kimaisha kupitia sanaa ya muziki ambapo hivi sasa mbali na kupata show mbalimbali hivi sasa anafahamiana na watu wengi.
Hadi hivi sasa bado Wema hajazungumzia swala hilo ambalo limezua gumzo kwa mashabiki wa muziki na filamu hapa nchini

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Mwimbaji wa ‘Tumetoka Mbali’, Linah Sanga ambaye aliahidi kuanzisha kipindi cha runinga mwezi wa nane mwaka jana, ameelezea sababu zilizompelekea yeye kushindwa kuitimiza ahadi hiyo kwa muda.
Akizungumza na muandishi wa tovuti ya Times Fm alisema alishindwa kutekeleza ahadi hiyo kwa wakati kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza kwa upande wa uongozi wake, ulioshauri kubadilika kwa ratiba hiyo, “Mimi na timu yangu (Crew) tulitegemea kukirusha hewani mwaka Jana ila uongozi uliona ni vizuri tuanze rasmi kukirusha mwaka huu.”
Amesema kipindi hicho cha Television alichokipa jina la 3D, kina lengo la kuwahamasisha wazazi wote nchini kutowalemaza watoto wao kwenye vipaji tu na kusahau masomo kwa kuwa anaamini elimu ndio msingi wa maisha bora.
Endapo kipindi hicho kitaanza, Linah ataingia kwenye orodha wasanii wa Tanzania wenye vipindi vyao binafsi kwenye vituo vya runinga wanaoshiriki moja kwa moja na kuonekana, kama Lady Jay Dee, Wema Sepetu na wengine.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Watu wengi wamekuwa wakiendelea kukumbwa na tatizo la kuoza kwa meno na kujikuta wakiishia kuwa na mapengo bila ya kujua chanzo cha kuharibika kwa meno hayo.
Kwa mujibu wa kaimu mgamga wa meno mkoa wa Mwanza Dr. Ismail Sarumbo wakati akifanya mahojiano na Muandishi Charles Urio katika kipindi cha Linda Afya yako cha Afya radio Mwanza alibainisha kuwa tatizo hili husababishwa na bacteria wa aina tofauti tofauti ambao kwa pamoja wanaitwa normal Flora wanaoishi katika mdomo wa binadamu.
Bakteria hao huharibu jino kwa kemikali ambayo wameitengeneza baada ya kukutana na mabaki ya vyakula katika meno.
Watu wengi hukumbwa na hali hii kutokana na kutokuwa na tabia ya kupiga mswaki mara baada ya chakula hali ambayo inaacha mabaki ya chakula katika meno hali ambayo inatufanya tuyaathiri meno yetu wenyewe.
Ili kuepuka ugonjwa huu hatuna budi kuchukua hatua ya kupiga mswaki mara kwa mara pindi tunapo maliza kula na kuyaaacha meno yetu yakiwa salama.
Kwa undani zaidi Download na umsikilize kaimu mganga wa meno Dr. Ismail Sarumbo

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii lady jaydee ametoa nafasi kwa mashabiki wake kumchagulia jina atakalotumia katika band yake ya machozi band.
Hatua hii ya lady jaydee inakuja kufuatia kuonekana kuchoka na jina hilo ambalo amedai limepitwa wakati.
Kupitia ukrasa wake wa face book msanii huyu ameandika kuwa anafikiria kubadilisha jina la machozi ambalo amedai kulitumia katika kipindi ambacho alikuwa analia

Lady Jaydee
"Nafikiria kubadilisha jina la band sababu Machozi Machozi niliolia zamani yashafutika. Mnashaurije???"

Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Msanii profesor jay amewakumbusha watu kuishi kwa upendo na kutobaguana ili kuishi kwa amani na furaha.
Kupitia ukurasa wake wa face book msanii huyu amepost picha inayomuonesha yeye akiwa amebeba mtoto ambaye ni abino pia inamuonesha msanii fid q na watu wengine watatu ambao kati yao wawili ni albino na kuandika maelezo yanayosisitiza kupiga vita ubaguzi na kuishi kwa upendo

Professor Jay
"BINADAMU wote ni sawa..Na tumeagizwa AMANI Na UPENDO, Mwenyezi Mungu awabariki sana! !!"
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)

Video ya wimbo wa "ZIPATE TUKUJUE" unaomilikiwa na wasnii kutoka jijini Mwanza King Silver,Op mtata na Natty E imeanza kushutiwa leo hii.
Akizungumza na Bongo20 mmoja wa wasanii hao msanii Op mtata ameeleza kuwa shughuli ya kuchukua vipande vya video ya wimbo zinaanza leo na kuwa hivi karibuni itakamilika.
Kuandaliwa kwa video hii  inayotarajiwa kuachiwa muda wowote itakapo kamilika inakuwa ni miongoni mwa malengo waliojiwekea wasanii hawa kwa mwaka huu.
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Shilole
Msanii wa muziki na filamu nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Shilole amesema anashangazwa na kitendo cha msanii mwenzake Baby Madaha kumsema vibaya mara kwa mara.
Akizungumza na Chanel 10 msanii huyu amesema yeye hana tatizo na msanii huyo lakini Baby Madaha amekuwa akimsema kila mara kitu ambacho anashindwa kuelewa kinatokana na nini.
Ameongeza kuwa yeye hana muda wa kupoteza kubishana na msanii huyo kwa kuwa anaamini hana tatizo na msanii huyo.
“Ni kama Baby Madaha anavyonizungumzia mimi, mmekua mkiona na wengine mliumia mkasema sana kwa nini ananizungumzia mimi. Baby Madaha sina tatizo naye lakini nashangaa amekuwa mtu wa kunizungumzia everyday, I don’t know why.” Amesema Baby Madaha.
Msanii huyu akaendelea kwa kumueleza msanii huyo kutomfuatilia kwa kuwa yeye hamfuatilii.

“Wewe mwanamke, mimi mwanamke mwenzio nafanya kazi, umeshaniona hata siku moja naenda kukuzungumzia somewhere? Muogope Mungu kukaa unamzungumzia mtu ambaye hana time, hana shida na wewe. Hebu tubadilike wanawake tupendane tuache kuzumziana vibaya.” Shilole ameeleza.
Bongo20 inaendelea kufuatilia chanzo cha wasanii hao kuingia katika uhusiano mbaya
Bongo 20 Blog ni blog ya kijamii inayokupa habari mbalimbali za kijamii pamoja na afya ikisimamiwa na Harith Jaha (Mr. Credit)
Cover la filamu mpya ya Dr.Cheni linalodaiwa kuchochea ushoga


Msanii wa filamu hapa nchini anayefahamika kwa jina la Dr. amejikuta katika wakati mgumu baada ya bodi ya filamu Tanzania kuzuia filamu yake mpya inayoitwa 'Nimekubali Kuolewa' kwa madai ya cover iliyotumika katika kasha la filamu hiyo inachochea ushoga.
Kufuatia madai hayo msanii huyo amesema kuwa