Shilole
Msanii wa muziki na filamu nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Shilole amesema anashangazwa na kitendo cha msanii mwenzake Baby Madaha kumsema vibaya mara kwa mara.
Akizungumza na Chanel 10 msanii huyu amesema yeye hana tatizo na msanii huyo lakini Baby Madaha amekuwa akimsema kila mara kitu ambacho anashindwa kuelewa kinatokana na nini.
Ameongeza kuwa yeye hana muda wa kupoteza kubishana na msanii huyo kwa kuwa anaamini hana tatizo na msanii huyo.
“Ni kama Baby Madaha anavyonizungumzia mimi, mmekua mkiona na wengine mliumia mkasema sana kwa nini ananizungumzia mimi. Baby Madaha sina tatizo naye lakini nashangaa amekuwa mtu wa kunizungumzia everyday, I don’t know why.” Amesema Baby Madaha.
Msanii huyu akaendelea kwa kumueleza msanii huyo kutomfuatilia kwa kuwa yeye hamfuatilii.

“Wewe mwanamke, mimi mwanamke mwenzio nafanya kazi, umeshaniona hata siku moja naenda kukuzungumzia somewhere? Muogope Mungu kukaa unamzungumzia mtu ambaye hana time, hana shida na wewe. Hebu tubadilike wanawake tupendane tuache kuzumziana vibaya.” Shilole ameeleza.
Bongo20 inaendelea kufuatilia chanzo cha wasanii hao kuingia katika uhusiano mbaya
Axact

Post A Comment: