Cover la filamu mpya ya Dr.Cheni linalodaiwa kuchochea ushoga


Msanii wa filamu hapa nchini anayefahamika kwa jina la Dr. amejikuta katika wakati mgumu baada ya bodi ya filamu Tanzania kuzuia filamu yake mpya inayoitwa 'Nimekubali Kuolewa' kwa madai ya cover iliyotumika katika kasha la filamu hiyo inachochea ushoga.
Kufuatia madai hayo msanii huyo amesema kuwa
bodi hiyo haikumtendea haki kwa kuwa filamu yake ina lengo zuri la kupinga ushoga na sio kuchochea.
Ameela bodi hiyo haikuangalia maudhui na badala yake imeangalia zaidi cover la filamu hiyo

“Eti ushoga wangu uko kwenye kujiremba sana, wamenionea, lengo letu ni kukemea na kupinga vikali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja, huwezi kuelimisha bila kuonesha madhara yake kwa vitendo kama ilivyo kwenye filamu hiyo. Amesema Dk Cheni.

Msanii huyu amekumbwa na hali hiyo ikiwa ni muendelezo wa bodi ya filamu kuzuia filamu ambazo inazitilia mashaka.
Hata hivyo bodi hii imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya wasanii wakidai haitendi haki.
Axact

Post A Comment: