Msanii Tunda Man ni mmoja kati ya wasanii ambao wamewahi kukumbwa na hatari ya kuaibika.
Akizungumza na Bongo20 msanii huyu amesimulia namna alivyonusurika kudhalilishwa baada ya kukosa pesa ya kulipia vinywaji pamoja na chakula alichotumia.
Msanii huyu alisema kuna siku alikwenda Kijitonyama katika kiwanja kimoja kwa ajili ya kula na kupata vinywaji,alipofika huko alikutana na baadhi ya jamaa zake ambapo waliungana na kuendelea kukamua.
Kwa muda wote wakiendelea kujiachia wale jamaa zake walikuwa wakitegemea pochi ya Tunda,kuna muda ulifika msanii huyu akaamua kuangalia alio lake kwa waleti ambapo hakukuta kitu na ndipo alipoanza kujiuliza ni nani wa kumsitiri na aibu ambayo inataka kumkumba.
Kwa bahati akapata wazo la kumtafuta Suma Lee ambaye kwa bahati alitokea na kumlipia.
Tunda man alieleza kuwa yote hayo yalimtokea akiwa tayari amekwisha kuwa msanii.
Post A Comment: