Msanii nguli wa Bongo fleva Proffesa Jay pamoja na msanii wa nyimbo zenye vionjo vya kiasili Mrisho Mpoto huenda wakatengeneza ladha mpya ya muziki kutokana na kukutana katika kazi moja.
Kupitia ukurawa wake wa mtandao wa kijamii wa face book msanii Proffesor Jay ameandika maelezo yanayoashiria wawili hao kuna kazi wanayoifanya kwa pamoja.
Msanii huyu mbali na maelezo hayo pia ame post picha inayomuonesha akiwa na Mpoto wakiwa katika studio ya Waite records inayomilikiwa na Mrisho Mpoto.

Nimemtembelea mjomba @mrisho mpoto kwenye studio yake ya WAITE RECORD. .. Mambo makubwa sana yanafuata. .STAY TUNED!!


Hatua hii ya ya wasanii hawa imeonesha kuungwa mkono na baadhi ya mashabiki ambao wameamua kuwapongeza.Hata hivyo bado wasanii hawa hawajaweka wazi ni kazi gani wanatarajia kuzifanya kwa pamoja.
Axact

Post A Comment: