Mkali wa RnB mwenye mashabiki wengi wanaopenda aina hiyo ya muziki hususani hapa Tanzania, ameweka wazi jinsi ambavyo analipwa zaidi kwa shows za nyumbani Tanzania kuliko shows za nje ambazo amepata mialiko.
Mkali huyo wa ‘Manenomaneno’ amefunguka katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm wakati akitambulisha rasmi wimbo wake ‘Umenichora’ aliofanya na Fundi Samweli na Joh Makini, na kuutoa mfano hai wa show yake atakayofanya Ujerumani, April  mwaka huu.
“Definitely, nyumbani kuna nguvu sana, mfano mimi mwezi wa nne nina show moja German, lakini hiyo show…inalipa vizuri, lakini trust me navyopata hapa kwenye show ya Bongo ni twice.” Amesema Ben Pol.
Ameeleza hiyo kuwa sababu ya kubadilika na kufanya RnB yenye vionjo vya kitanzania, na kuwashauri wasanii wengine kufanya muziki wa nyumbani ili waweze kupata shows zaidi nje zitakazowalipa pesa nyingi zaidi.
 “Kwa sababu...unajua shows nyingi tunaenda kufanya kama nje, kama unapiga muziki wenye flavour ya nje, ni shida sana kufanya ile classic RnB halafu ukafanya kuliko R Kelly. Kwa mantiki hiyo, tufanye muziki wa nyumbani ili watu wa nje wakisikiliza waseme mbona hatuwezi kufanya muziki kama wa yule. Kwa hiyo kama wakiona kama haiwezi wanaweza kui-add kwenye stream yao kwa kuwa wao wanaona hawaiwezi.”
Axact

Post A Comment: