Kumekuwa na tetesi zinazosema kuwa msanii Wema Sepetu ana uhusiano wa kimapenzi na msanii aliye chini ya kampuni yake ya Endless fame msanii Mirror.
Kufuatia uvumi huo msanii Mirror ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia tetesi hizo ambapo amekanusha na kudai kuwa hazina ukweli.
Ameeleza yeye na Wema ni kama ndugu na hakuna chochote kinachoendelea zaidi ya uhusiano wa kazi.
Ameongeza kuwa Wema amekuwa ni mtu mzuri kwake kwa kuwa amemsaidia kimaisha kupitia sanaa ya muziki ambapo hivi sasa mbali na kupata show mbalimbali hivi sasa anafahamiana na watu wengi.
Hadi hivi sasa bado Wema hajazungumzia swala hilo ambalo limezua gumzo kwa mashabiki wa muziki na filamu hapa nchini

Axact

Post A Comment: