Msanii kutoka nchini Tanzania Young d Amesema baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na mtu anayetumia jina lake face book kutapeli watu msanii huyu amedai kupata suluhisho la tapeli huyo.
Msanii huyu ameeleza kuwa ni kwa muda mrefu amekuwa akitafuta namna ya kumtia hatiani mtu huyo bila mafanikio kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha.
Ameeleza hivi sasa tayari amekwishapata mtu ambaye ametapeliwa na mtu huyo kama alivyoshauriwa na askari na kuwa huyo ndiye atakayetia nguvu katika kesi hiyo.
Amefunguka zaidi kuwa pamoja na kumpata mtu huyo aliyetapeliwa tayari ana mwanasheria ambaye atasaidiana naye katika kumfungulia kesi mtu huyo.
Msanii huyu amekwisha fanya jitihada za kumpata mtu huyo anayemuita tapeli kwa kuripoti polisi ikiwa ni pamoja na kutangaza kwa watu kuwa yeyote anayemfahamu mtu huyo ampe taarifa,hata hivyo juhudi zake hazikuonesha mafanikio yoyote.
Post A Comment: