MSANII JB KUINUA WASANII WADOGO
Msanii kutoka Bongo
movie Jacob Steven au JB amesema ana mpango wa kuwainua wasanii wanaochipukia.
Akizungumza mapema wiki
hii msanii huyu amesema yeye na kampuni ya Jerusalem wamefikia uamuzi huo baada
ya kuona kuna watu wana vipaji na wanahitaji kusaidia hivyo yeye ameona kuna
haja ya kufanya hivyo.
“sisi Jerusalem company
tunajua Mungu alipotuweka alituweka ili tushike watu wengine mikono na mpaka
sasa hivi nime sign kwenye contract yangu filamu za aina mbili. Kuna filamu
ambazo mimi nitashiriki na kuna zingine sitoshiriki kabisa nita direct na ku
produce nita tupa ela kuzifanya hizo film kwa ajili ya hawa under grounds”
alisema JB.
Jb aliongeza zaidi kuwa
kuanzia mwakani atakuwa akitoa filamu tatu ambazo atazicheza yeye mwenyewe na
nyingine kumi atakazotoa zitachezwa na wasanii wengine wadogo huku yeye
akizisimamia.
Katika kipindi cha
miaka ya hivi karibuni Jb amekuwa ni mmoja wa wasanii wa filamu wa kubwa hapa
nchini na wanaokubalika kutokana na uchezaji wao wa filamu na ni mmoja kati ya wasanii waliopata tuzo mwaka huu kupitia movi inayojulikana kwa jina la Nakwenda kwa Mwanangu aliyocheza na msanii wa vichekesho King Majuto huku mzee huyo kuchukua tuzo ya mchekeshaji bora kwa kupitia movi hiyo.
Tuzo nyingine aliyoipata ni muigizaji bora wa kiume katika tuzo zilizoandaliwa na kampuni ya steps.
Post A Comment: