Taarifa kutoka kwa msanii Roma zinasema mama yake mzazi si mpenzi sana wa nyimbo zake na badala yakeanawakubali zaidi wasanii Barnaba,Linex,Bushoke na Ben Pol.Habari zaidi zinasema mama huyo pamoja na kupendea nyimbo za wasanii hao kuna jambo linamkera kwa Linex.Akizungumzia jambo hilo msanii Roma amesema mama yake anakerwa na milegezo ya Linex ambapo anadai ni vyema akawa anavaa kawaida.Kwa mjibu wa timesfm blog msanii huyu ameeleza kuwa anadhani kuwa mama yake sio shabiki wake kutokana na kutosikiliza nyimbo za mwanae kama anavyosikiliza za wasanii wengine
Post A Comment: