Ney wa Mitego |
Katika mahojiano na timse fm Ney wa Mitego alisema kufuatia tukio hilo atamdharau Ostaz kuliko mtu yeyote hapa duniani.
Aliendelea kufunguka zaidi kwa kueleza kitendo hicho kimemgusa zaidi kuliko hata Pnc mwenyewe.
Mimi tangu nilipoona hizo picha nilisema siwezi kumpenda hata siku moja, hata salamu yangu siwezi kumpa. Siwezi kumheshimu hata kidogo. Nitamdharau kuliko kitu chochote, kuliko mtu yeyote aliyewahi kunikosea sana. Ila katika watu ambao waliowahi kunikosea, nafikiri mimi Ostaz Juma amenikosea kupita maelezo. Kuliko alivyomkosea PNC mwenyewe.” Alifunguka Ney
Msanii huyu anauungana na baadhi ya wasanii pamoja na wadau wa muziki ambao walionekana kukerwa na kitendo hicho wakidai ni udhalilishaji kwa wasanii.
Post A Comment: