Mmiliki wa shindano la Bongo Star Search nchini Tanzania Rita Paulsen maarufu kama madam Rita ameamua kuwafungukia baadhi ya watu ambao wwanaitumia mitandao ya kija mii vibaya.
Kupitia ukurasa wake wa face book mama huyo ameandika maelezo yanayoashiria kupinga watu hao ambao mara nyingi huchafua majina ya watu kwa kuandika vitu visivyo faa.
“Hivi sasa mitandao ya kijamii inawezesha watu kusema kile wanachokifikira na kutaka sauti na hoja zao kusikilizwa. Lakini wengine wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutusi na kuchafua majina ya watu. Huo kwakweli sio uungwana kwani hamna faida yoyote itakayopatikana pindi unapomchafulia mtu mwingine jina lake.

Ni mtazamo tu!. Nawatakia Alhamisi njema wadau” Aliandika Madam Rita
Imekuwa ni kwaida kwa baadhi ya watu kuchafua watu au kupost picha mbaya katika mitandao ya kijamii kiasi cha kusumbua watu wengine.
Axact

Post A Comment: