Baada ya kiongozi wa G-Unit, 50 Cent kumdhihaki hasimu wake wa muda mrefu, Rick Ross kwa kupost picha zinazoonesha kuwa huenda ni shoga, wengi walijua tayari moto umewashwa na kilichobaki kusubiri nini atakachofanya Rick Ross.

Lakini kwa mujibu wa chanzo cha mtandao wa TMZ, rapper huyo ambaye jina lake halisi ni William Leonard Robert II, hataupoteza muda wake kumjibu rapper huyo na kueleza sababu kuwa anamuona 50 Cent hana umuhimu kwake.

Imeelezwa kuwa Rick Ross amepanga kuiacha hiyo issue ipite kimya kimya na yeye aendelee kujikita katika masuala muhimu ya kutengeneza ngoma kali.

Jumapili iliyopita, 50 Cent alipost kwenye Instagram picha inayomuonesha Rick Ross akimsogelea P.Diddy kama vile wanataka ku-kiss na akaandika kwa ufupi, “something ain’t right’.
Axact

Post A Comment: